BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTANGAZAJI WA ITV UFOO SARO AIBUKIA KKKT NA KUTOA NENO HUKU MACHOZI YAKIMBUBUJIKA KUFUATIA SAKATA LAKE LA KUNUSURIKA KIFO BAADA YA KUFUATULIWA RISASI NA MZAZI MWENZAKE 2013.

1535545_694056513980529_1677684344_n

MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha ITV Ufoo Saro ambaye Oktoba 13 zilisambaa taarifa zinazomhusu yeye na familia yake, taarifa hizi zilikuwa za kupigwa risasi na kujeruhiwa na mzazi mwenzake Anthery Mushi.

Ufoo saro jana amefanya ibada na kusema ‘Namshukuru Mungu kwa kumponya’ hii ni mara ya kwanza kwa Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.ufoo
Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba Jimbo la Magharibi Ufoo huku akitokwa na machozi na wakati mwingine kushindwa kuzungumza alisema ‘Ni miujiza tu ya Mungu yeye kunifanya mimi kuwa hai leo’.


Mtangazaji huyo ambaye alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili hospital aliwashukuru watu wote waliomtia moyo na kumsaidia kipindi chote alichokuwa mgonjwa ‘Sina cha kuwalipa,ninawashukuru sana kwa wema wenu pia kwa kuniombea Mungu ni mkubwa na amenipigania naendelea vizuri kwa sasa Mungu alinisimamia na nyinyi pia mliniombea hakika sina budi kushukuru kwa kila jambo,nitasoma zaburi ya 146 katika Biblia Takatifu ili kumshukuru Mungu kwa kunisaidia’.


Ufoo alisema kuwa ameamua kumshukuru Mungu kwa sababu siyo watu wote wanaopata matatizo kama yake na wakapona.


Mchungaji wa kanisa hilo Joseph Maseghe aliyeongoza misa hiyo iliyofanyika asubuhi ya leo alisema Mungu hakupanga Ufoo afariki dunia kwa kupigwa risasi ‘Mungu bado anakuhitaji hakupanga ndiyo maana upo nasi leo hautakiwi kulia huu ni mwanzo wa maisha yako mengine usilie unachotakiwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo’.a;imalizia mchungaji huyo.


Misa hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wafanyakazi wa ITV pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Grace Kihwelu akiwemo na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) John Heche,baada ya kukamilika kwa misa hiyo ndugu na marafiki wa karibu wa Ufoo walijumuika pamoja kwenye hafla fupi ya chakula cha mchana.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: