BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAMKE AZIDI KUTOA PIPI ZA MADAWA YA KULEVYA AINA YA HEROIN, MPAKA SASA TAYARI AMETOA PIPI 72 KWA NJIA YA HAJA KUBWA JIJINI DAR ES SALAAM.


Kamishna wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa.


DAR ES SALAAM. 
MWANAMKE aliyekamatwa juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, yupo chini ya ulinzi wa polisi huku akiendelea kutoa pipi za heroin kupitia njia ya haja kubwa.


Hadi kufikia jana mchana alikuwa ametoa pipi 72.
Mtuhumiwa huyo, alikamatwa juzi akiwa mbioni kwenda China, kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Hatua hiyo ilikuja baada ya kuhisiwa kumeza kete hizo.
Kamishna wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema mwanamke huyo anaendelea kutoa pipi hizo.

“Anaendelea kutoa kete zaidi na ndiyo maana hatukuweza kusema idadi kamili ya mzigo alioumeza kwa sababu wakati mwingine wanadanganya, hawasemi ukweli kuhusu kiasi cha mzigo walioumeza, wana mbinu nyingi hawa,” alisema Nzowa
Alisema baada ya kushikwa mtuhumiwa aliwaambia polisi kuwa amemeza pipi 61, lakini baadaye alisema amemeza pipi 40.

Alisema ukweli kamili utabainika baada ya upelelezi.
Alisema mtuhumiwa huyo pia amekataa kuwataja watu waliomtuma licha ya kubanwa kwa mbinu zote.

Nzowa pia alisema, watuhumiwa wanaomeza dawa za kulevya huzitoa pipi hizo kwa njia ya haja kubwa ambapo mwili wenyewe kupitia mfumo wake, unazitoa wakati mtu anapokula.

“Hatuwapi kitu chochote cha kuwafanya wazitoe, lakini anapoendelea kukaa, akila chakula basi na zenyewe kupitia mfumo wa mwili hutoka. Ndiyo maana huyu mwanamke mpaka sasa anaendelea kuzitoa taratibu, mpaka zitakapoisha,” alisema.

Nzowa alisema endapo itatokea pipi hizo hazikufungwa vyema zinaweza kupasukia tumboni na aliyemeza kupoteza maisha na kwamba kwa mtuhumiwa jinsi anavyozitoa taratibu upo uwezekano wa kupasuka.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: