BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHULE YAKOSA CHOO KWA MIAKA MITATU, VIONGOZI WA KIJIJI WATIMULIWA KAZI KUTOKANA NA UZEMBE MKOANI RUKWA.

 
WAKAZI wa Kijiji cha Chalatila, Kata ya Kate, Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, wameukataa uongozi wa kijiji hicho baada ya kushindwa kusimamia ujenzi wa choo cha shule msingi kijijini hapo hivyo kuhatarisha afya za wanafunzi na walimu. 



Shule hiyo inadaiwa kukosa choo miaka mitatu hadi sasa ambapo aumuzi huo ulifikiwa baada ya wananchi kumtaka Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo, Bw. Gilbert Masime,aitishe mkutano wa wazazi ili watafute ufumbuzi. 



Katika mkutano huo, wananchi hao waliamua kuwakataa viongozi wa kijiji ambao ni Mwenyekiti Bw. Linus Masumbuko na Ofisa Mtendaji, Bw. Octavian Sanka wakidai wameshindwa kutekeleza majukumu yao na kufanikisha ujenzi wa choo. 



Wananchi hao walimchagua Bw. Masime kuwa Mwenyekiti mpya na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Beatus Nandy waweze kuanzisha kampeni ya kukusanya michango ya wananchi ili kuchangia nguvu zao katika ujenzi wa choo. 




Alipotakiwa kulitolea ufafanuzi suala hilo, Kaimu Ofisa Elimu wilayani humo ambaye pia ni Ofisa Elimu ya Watu Wazima, Bw. Raphael Siumbu, alisema wao kama idara walitoa maelekezo kwenye Serikali ya kijiji lakini viongozi wameshindwa kulisimamia na wamepokea maamuzi ya wananchi. 



"Tumepokea maamuzi ya wananchi kuwakataa viongozi wao,tulikwenda katika shule yao kujua sababu zinazokwamisha wasiwe na choo...licha ya kubaini udhaifu wa viongozi wa kijiji tuliamua kuubariki uongozi wa muda uliyochukua madaraka. 



"Hivi sasa tunaandaa ripoti ambayo itakabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya aweze kutoa maamuzi juu ya viongozi hawa," alisema. 



Naye Ofisa Afya wa Wilaya hiyo, Anselmo Kapandila, alisema baada ya kupata ripoti kuwa shule hiyo haina choo, alikwenda kujionea na kama itashindwa kukijenga hadi Januari 13 mwaka huu, atalazimika kuifunga. 




"Nimewapatia mbinu mbalimbali za dharura ili kukamilisha ujenzi wa choo cha muda kabla shule hazijafunguliwa kama watashindwa nitaifunga," alisema. 



Mwenyekiti wa kijiji hicho, Masumbuko ambaye aliondolewa madrakani, alisema kusimamishwa kwake kumetokana na uzumbe wa Ofisa Mtendaji, Bw. Sanka ambaye naye alimtuhumu Mwenyekiti wake na kudai hawelewani muda mrefu. 



Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Kimulika Galikunga, alikiri kupata taarifa hiyo na kuongeza kuwa, anajiandaa kutoa maamuzi kwa viongozi wa kijiji lakini lengo la halmashauri ni kuona choo kinajengwa katika shule hiyo. MAJIRA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: