BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAARIFA MPYA !!! BENDI YA MUZIKI WA DANSI YA TWANGA PEPETA YAMPOTEZA MPIGA TUMBA MAHILI MC D ALIYEFARIKI DUNIA USIKU WA JANUARI 27 MWAKA HUU.

KAMA mfatiliaji wa muziki wa Dansi Tanzania, jina la Mc D si jina geni kwako, jina lake halisi ni Masoud Mohamed, ni mpiga tumba kutoka bendi ya African Stars Band’Twanga pepeta’ taarifa hizi zimetangazwa usiku na kuthibitishwa na msemaji wa Twanga pepeta Hassan Rehani.



Taarifa zaidi inasema kuwa Mc D alikua  Moshi kwa matibabu zaidi ya miezi miwili na hali yake iliendelea vizuri hadi usiku wa jana wa January 27 hali yake ilipobadilika na kufariki dunia.


Wiki chache nyuma ilisemekana Mc D alikua akiendelea vizuri kwani hatua ngumu ya dozi ya kali ya kifua kikuuu alikua kaivuka na sasa alikua amebadilishiwa dawa, aliongea kwa matumaini makubwa kuwa atarejea jukwaani muda si mrefu.


Miongoni mwa bendi alizozitumikia Mcd enzi ya uhai wake ni pamoja na Diamond Sound, Mashujaa Band na Twanga pepeta.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: