DAR ES SALAAM.
WAFUASI wa Chadema wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wanaounga mkono uongozi wa juu, jana walitwangana tena muda mfupi baada ya kuondoka eneo la Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
WAFUASI wa Chadema wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wanaounga mkono uongozi wa juu, jana walitwangana tena muda mfupi baada ya kuondoka eneo la Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Tukio hilo limetokea huku Mahakama hiyo
ikiahirisha hadi leo, kutoa uamuzi wa maombi ya Zitto kuzuia kujadiliwa
na Kamati Kuu ya Chadema.
Katika maombi hayo namba 1 ya mwaka 2014, Zitto
ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, anaiomba Mahakama iizuie
Kamati Kuu ya Chadema kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu
uanachama wake hadi kesi yake ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo
itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Uamuzi wa maombi hayo ulipangwa kutolewa jana na
Jaji John Utamwa ambaye hata hivyo, alisema alikuwa hajamaliza kuandika
uamuzi huo na kuahirisha shauri hilo hadi leo mchana.
Maombi hayo ya Zitto ya zuio la muda la kujadiliwa
na kuchukuliwa uamuzi wowote kuhusu uanachama wake yametokana na kesi
ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya
Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Katika kesi hiyo, Zitto pia anaiomba Mahakama Kuu
imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie mwenendo na taarifa za kikao cha
Kamati Kuu za kumvua nyadhifa zake zote alizokuwa nazo ndani ya chama
na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake
ya ubunge wa Kigoma Kaskazini.
Mapigano
Baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, wanachama wa
makundi yote waliondoka eneo la Mahakama wakiendelea kuimba na
kushangilia lakini walipofika eneo la Mahakama ya Rufani ghafla walianza
kupigana ngumi na mawe. Baadhi yao walikamatwa na askari kutokana na
vurugu hizo.
Awali, wafuasi hao walifika mapema asubuhi katika viwanja vya Mahakama tayari kusikiliza uamuzi huo.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa na askari polisi
wakiwamo wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliokuwa na silaha
pamoja na mabomu ya machozi walikuwa wametanda.
Pia kulikuwa na askari wa Kikosi cha Mbwa pamoja na gari la maji ya kuwasha.
Licha ya kuwahi, ni wafuasi wachache walioruhusiwa
kuingia ndani ya u`kumbi wa Mahakama tena baada ya kuandikisha majina
yao huku wakitambuliwa na viongozi wao waliokuwapo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment