MATUKIO ya utekaji watu, kuwatesa na kuwatelekeza,yameanza tena baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, Bw. Joseph Yona, kutekwa, kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili na kutupwa eneo la Ununio, Tegeta, Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kumakia jana baada ya watekaji hao, kumkuta Bw. Yona eneo Mtoni kwa Azizi Ally, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.
Bw. Yona alikuwa amekaa katika tawi la chama hicho na watu wengine sita wakiwa katika mazungumzo ya kawaida.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika Kitengo cha Taasisi ya Mifupa (MOI),
kilichopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambako amelazwa,
Bw. Yona alisema sababu ya kutekwa kwake na kutezwa ni baada ya kuitisha
mkutano na wahandishi wa habari.
"Mkutano huu niliuhitisha katika Hoteli ya Lamada, Ilala,Dar es Salaam uliokuwa ukijadili sakata la kuvuliwa uongozi Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe katika chama ndipo nilipoanza kutishwa kila wakati.
"Uongozi wa chama Makao Makuu ulitaka kuning'oa katika nafasi yangu lakini Kamati ya Utendaji ilikataa na kudai hawaoni kosa langu ni lipi...lilitoka agizo kwa viongozi wakuu wa chama kutaka ofisi yangu Temeke ifungwe," alisema.
Aliongeza kuwa, siku ya tukio saa 5 usiku akiwa eneo la Mtoni kwa Azizi Ally akizungumza na watu watatu, aliona kundi la watu sita likifika eneo hilo na kusema wanataka kumkamata yeye si watu wengine aliokuwa amekaa nao.
Bw. Yona alisema, alipowauliza wametumwa na nani kumkamata walidai ni maagizo ya viongozi wakuu wa CHADEMA, kutokana na mkakati wake wa kumuunga mkono Bw. Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho.
"Walinikamata na kudai wananipeleka Kituo cha Polisi Kati kwenda kutoa maelezo zaidi lakini nilishangaa kuona gari likipita kituoni na kwenda eneo ambalo sikulijua.
"Tulipofika eneo ambalo sikulifahamu, nilivuliwa fulana na kuzibwa machoni, walianza kunipiga na kunihoji wakinitaka niachane na shughuli za chama ili wasiniue," alisema.
Aliongeza kuwa, hakuweza kuwajibu kitu bali aliwaambia kuwa, kama wanataka maelezo zaidi kuhusu Kabwe waende wakamuulize mwenyewe kwani yeye hawezi kumsemea.
"Nilipojibu hivyo, mmoka kati ya watekaji alinipiga na kitu chenye ncha kali kichwani akiwa amenibinya sehemu zangu za siri...nilisikia maumivu makali nikawambia kwa nini mnaniua na mimi nina familia kama nyinyi.
"Muda huo tayari nilikuwa nimepigwa na kitu kizito, kupoteza fahamu hivyo walikimbia wakijua nimepoteza maisha, nilikuja kuamka saa 10 alfajiri na kujikuta niko peke yangu, nguo zangu zilikuwa zimetapakaa damu," alisema Bw. Yona.
Alisema baada ya kujitambua, alikwenda kugonga hodi katika nyumba ziliyopo jirani na eneo hilo ili kuomba msaada.
"Nilijitahidi kugonga milango milangu katika nyumba tatu lakini sikufunguliwa hivyo niliamua kujisogeza kidogokidogo ili nisubiri kukuche niombe msaada kwa watu wengine.
"Ilipofika saa 11
alfajiri, katia nyumba nilizogonga mlango kuna mtu alitoka, kunifuata na
kuniuliza shida yangu ndipo nikamwambia...anilitaka nitaje namba ya mtu
wangu wa karibu nikampa ya mdogo wake anaitwa Ayubu," alisema.
MOI wazungumza
Msemaji wa MOI, Bw. Patrick Mvungi, alisema walimpokea Bw. Yona saa 5 asubuhi akitokea MNH akiwa tayari amefanyiwa kipimo cha TC-SCAN hivyo bado anaendelea na matibabu.
CHADEMA wasikitishwa Wakati huo huo, taarifa iliyotolewa na CHADEMA Makao Makuu, imesema imepokea taarifa za kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa Bw. Yona kwa mshtuko mkubwa.
Taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano, ilisema
tukio hilo la kihuni, mengine ya namna hiyo yenye lengo la kuendeleza
ukatili kwa binadamu
wanalikemea kwa nguvu zote.
"Katika hatua ya sasa, chama kinalitaka Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wa tukio la kutekwa, kuteswa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Wilaya ya Temeke ili ukweli ujulikane na haki itendeke kwa sheria kuchukua mkondo wake.
"Tunawakata wanachama na Watanzania kwa ujumla, kutulia hasa watu wenye hila na malengo yao, wanapoanza kukihusisha chama na tukio hili...pamoja na mtu yeyote kuwa kiongozi wa chama, bado anayo maisha yake na uhusiano na watu wengine katika jamii," ilisema taarifa hiyo.
Iliongeza kuwa, Jeshi la Polisi linapaswa kuyachukulia uzito unaostahili matukio ya namna hiyo ambayo yameanza kuota mizizi kutokana na watu waovu kutochukuliwa hatua za kisheria ambazo zingesaidia kuzuia yasitokee tena.
Taarifa hiyo ilisema
Watanzania bado wanakumbuka kuwa,hadi sasa jeshi hilo limeshindwa kutoa
taarifa za kina, kuchukua hatua za kisheria ambazo zingesaidia ukweli
kujulikana na haki kutendeka katika matukio ya kutekwa na kuteswa kwa
kiongoziwa madaktari Dk. Steven Ulimboka na Mwenyekiti wa Jukwaa
la Wahariri, Bw. Absalom Kibanda.
"Ukweli ungepatikana, ingesaidia kuzuia matukio mengine kutokea na kuendelea kutokea...mwendelezo huu unatokana na Jeshi la Polisi kushindwa kuwajibika ipasavyo katika matukio mengine ya namna hii, watu waovu wanaweza kutumia mwanya wa kinachoendelea ndani ya CHADEMA kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanachama wasio waadilifu," iliongeza taarifa hiyo.
Alisisitiza kuwa, watu hao wanaweza kutumia mwanya huo kufanya matukio ya namna hiyo ili kujenga taswira ya kukihusisha chama na uhuni unaobeba kila sifa ya kuitwa ukatili dhidi ya binadamu.
Polisi watoa tamko
Kutokana na tukio la kutekwa Bw. Yona, ambaye ni kitaaluma ni Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Elimu (DUCE), Dar es Salaam, kupigwa na kujeruhiwa, Jeshi la Polisi Kanda
0 comments:
Post a Comment