Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal (katikati) akiwa na Waziri mkuu Mizengo Kayanda Peter Pinda kushoto na Mzee Gabriel Tuppa wakiatafakari jambo wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa wa mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa.
Mvua yamkwamisha JK mazishi ya Tuppa.
NA MTANDA BLOG, MOROGORO
RAIS Jakaya Kikwete ameshindwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tuppa baada ya helikopta aliyopanda kwenda kushiriki mazishi hayo kushindwa kuendelea na safari kutokana na hali mbaya ya hewa.

Tuppa aliyefariki katikati ya wiki hii kwa ugonjwa
wa shinikizo la damu, alizikwa jana nyumbani kwake, Kasiki Wilaya ya
Kilosa Morogoro.
Akizungumza wakati wa salamu za rambirambi katika
mazishi hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema Rais Kikwete alikuwa
kwenye ratiba ya kushiriki mazishi hayo.
Aliongeza: “Ameshindwa kuja baada ya helikopta
aliyopanda kushindwa kupita anga la Mkoa wa Pwani kutokana na mvua kubwa
iliyoambatana na upepo na radi.”
Kutokana na hali hiyo, helikopta hiyo ililazimika
kurejea jijini Dar es Salaam salama na Rais Kikwete kuendelea na
shughuli zingine.
Akifafanua, Pinda alisema: “Baada ya hali kuwa
mbaya anga la Mkoa wa Pwani, rubani alijaribu kutumia njia mbadala ya
kufika Morogoro kwa kuzunguka eneo hilo hadi Bagamoyo, lakini hali
iliendelea kuwa hivyo.”
“Ilishindikana hata baada ya kujaribu kupita njia
nyingine, hali ya hewa ilikuwa mbaya sana, ilikuwa vigumu kuendelea na
safari ya kuja Morogoro,” alisema Pinda.
“Katika ratiba ya mazishi, Rais Kikwete alipangwa
kushiriki, lakini ameshindwa baada ya hali ya hewa kuchafuka kutokana na
ukungu uliotanda sehemu kubwa angani,” alisisitiza Pinda.
Naye Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro,
Telesphor Mkude aliwataka waumini wa madhehebu mbalimbali nchini kutoa
ushirikiano kwa kuwaombea Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ili waweze
kutoka na maoni yenye taswira ya masilahi ya taifa.
Mkude alisema kila Mtanzania awe macho katika
vikao vya kupitisha Katiba. “Ni vizuri kila mmoja akafuatilia
kinachoendelea Dodoma. Hii ni kwa faida yetu wote,” alisema.
“Siku ya leo ni siku ya majonzi kwa familia ya
marehemu na Wanakilosa kwa jumla, lakini siyo na Serikali pia kwani
imeondokewa na mtu muhimu sana na shupavu,” alisema Askofu Mkude.
Mazishi ya Tuppa yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefuni, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka, Stephen Wassira na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.

0 comments:
Post a Comment