BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC, MTIBWA SUGAR NAMNA WALIVYOMDEBWEDO LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA 2013/2014, WAPOTEZA MAKALI YAO.

Mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Jamal Mnyate (katikati) akijaribu kufunga bao huku akizongwa na beki wa JKT Ruvu George Minja kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa chamazi jijini Dar es Salaam. JKT Ruvu ilishinda 2-1. Picha na Michael Matemanga.

MBEYA.
NDOTO ya Simba kuwania ubingwa msimu huu imezidi kudidimia baada ya kulazimishwa sare 0-0 na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, huku JKT Ruvu ikiwachapa Mtibwa Sugar 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Kwa matokeo hayo Simba imebaki katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 21, wakiachwa kwa pointi nne na vinara Azam (40), huku Mbeya City wakiwa nafasi ya pili (39) na Yanga ipo nafasi ya tatu (38) wakiwa na mechi nne mkononi.


Katika mchezo huo Simba imeendeleza rekodi yake mbaya mikoani katika mzunguko huu baada ya kupata pointi tatu katika mechi sita ilizocheza nje ya Dar es Salaam.


Wenyeji Prisons walicheza kwa kujiamini katika muda wote wa mchezo huo kulinganisha na Simba ambao walionekana kukosa utulivu kila walipofika golini kwa wapinzani wao.


Prisons walipiga mashuti tisa golini yaliyolenga goli wakati Simba wenyewe walipiga mashuti manne tu. Dakika 30, beki wa Prisons, Nurdin Chona alipasuka juu ya jicho baada ya kugongana na Amisi Tambwe ambaye naye alipasuka kisogoni na kulazimika wachezaji wote wawili kwenda nje kutibiwa kabla ya kurejea uwanjani.


Mshambuliaji wa Prisons, Frank William alikosa bao la wazi baada ya kipa wa Simba Berko kutema na kupiga shuti lake nje ya uwanja katika dakika 38.


Chamazi, Katika mchezo huo mabao ya Ruvu yalifungwa na Kalage Gunda na Amosi Mgisa wakati lile la kufutia machozi la Mtibwa lilifungwa na Vicent Barbanas.


JKT Ruvu walipata bao la kuongoza kupitia kwa Gunda dakika 38, baada ya kupiga shuti akiwa nje ya 18.


Mshambuliaji wa JKT Ruvu, Haruna Adolf alikosa penalti dakika 59, baada ya Said Mkopi kuangushwa kwenye eneo la hatari na mwamuzi Jacob Adongo kuamuru penalti hiyo.


Mtibwa Sugar walisawazisha bao hilo dakika 70 kupitia mshambuliaji wake Barnabas kwa shuti la umbali wa mita 20 kabla ya Mgisa aliyeingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Kalage Gunda aliipatia Ruvu bao la pili dakika 75 kwa kumlamba chenga kipa wa Mtibwa Sugar, Hussein Sharif kabla ya kufunga goli hilo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: