BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WALEMAVU WASIOONA WAPATA MAFUNZO YA KUVUKA SEHEMU ZENYE VIKWAZO NA FIMBO NYEUPE MOROGORO.

Mwalimu mtalaam wasioona kutoka wilaya ya Kilosa, Japhet Magila kushoto akimwangalia mkufunzi wa chuo cha ualimu Kigurunyembe, Eliwaja Jacob wakati wa mafunzo ya kuvuka sehemu zenye vikwazo kwa walemavu wasioona yaliyofanyika mara baada ya kukabidhiwa fimbo nyeupe na shirika la Site Sever la jijini Dar es Salaam ili kuwajengea uwezo wa kutembea na kuondokana na utegemezi wakati wa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine kata ya Sultan Area mkoani Morogoro.
PICHA/MTANDA BLOG.

Mwalimu mtalaam wasioona kutoka wilaya ya Kilosa, Japhet Magila kushoto akimwangalia wa wanafunzi katika mafunzo ya kuvuka sehemu zenye vikwazo kwa walemavu wasioona.
Mwalimu mtalaam wasioona kutoka wilaya ya Kilosa, Japhet Magila kulia akiwaongozakuvuka barabara wakati wa mafunzo ya kuvuka sehemu zenye vikwazo kwa walemavu wasioona yaliyofanyika mara baada ya kukabidhiwa fimbo nyeupe na shirika la Site Sever la jijini Dar es Salaam ili kuwajengea uwezo wa kutembea na kuondokana na utegemezi wakati wa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine kata ya Sultan Area mkoani Morogoro.


 
Na MTANDA BLOG, MOROGORO.
ZAIDI ya walemavu 20 wasioona kati ya 80 katika Manispaa ya Morogoro wamepatiwa mafunzo ya awali ya matumizi sahihi ya fimbo nyeupe huku kundi hilo likikabiliwa na changamoto mbalimbali mkoani hapa.Akizungumza wakati wa mafunzo kwa walemavu wasioona kutoka kata nne za Manispaa ya Morogoro, Mwenyekiti wa chama cha wasioona Tanzania mkoani Morogoro, Godfrey Omari alisema kuwa kundi hilo la walemavu linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa fimbo nyeupe.


Omari alisema kuwa kwa sasa ni walemavu wasioona 25 ndiyo waliopata mafunzo ya awali ya matumizi sahihi ya fimbo nyeupe huku 75 wakikosa fimbo hizo ambazo zinamwezesha mlemavu huyo kutembea bila kuwa na mwongozaji.


“Sisi walemavu tusioona tuna changamoto nyingi lakini changamoto kubwa ni ya ukosefu wa fimbo nyeupe ambayo kila mlemavu asiyeona itamsaidia na kumpa faida ya kutembea bila ya kuwa na mwongozaji kwani mwenye fimbo hiyo anaondokana na utegemezi,”alisema Omari.


Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Mwalimu Mtaalam wasioona ambaye ni Mratibu Elimu kata ya Kasiki na Mbumi wilaya ya Kilosa, Japhet Magila ambaye alisema kuwa mafunzo yanaendeshwa kwa awamu tofauti ambapo awamu ya kwanza yalifanyika mwaka 2012 ikijumuisha walemavu 10.


Mratibu uyo pia alisema mwaka huu 2014 mafunzo kama hayo yamehusisha walemavu 15 na kufanya idadi yao kuwa 25 kati ya 80 ambao hawajapatiwa mafunzo ya kutumia fimbo nyeupe.


Magila alisema kuwa mpaka sasa fimbo 20 zimeweza kutolewa na shirika la Site Sever la jijini Dar es Salaam pamoja na kuendesha mafunzo kwa walemavu hao wasioona na kuwafanya kuwa na uwezo wa kutembea na kuondokana na utegemezi wakati wa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: