BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAUMINI WA MADHEHEBU YA DIN I WAOMBWA KULIOMBEA BUNGE MAALUM LA KATIBA ILI KUONDOA UCHAFU ULIOPO NDANI YA BUNGE DODOMA.


WAUMINI wa madhehebu mbalimbali ya dini wametakiwa kuliombea Bunge maalumu la katiba ili Mungu aingilie kati na kuondoa uchafu uliopo ndani ya Bunge. Mbunge wa Jimbo la Busanda Mkoa wa Geita, Lolena Bukwimba alitoa kauli hyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza. Wanawake kutoka madhehebu mbalimbali ya dini kwenye maadhimisho ya siku ya maombi ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kanisa la Anglikana Usharika wa Mlimwa mjini hapa.

Mbunge huyo alisema msaada mkubwa wanaoutegemea kuondoa uchafu huo ni maombi ambayo tunayoyaomba kutoka kwa waumini mbalimbali ambao wana dhamana kubwa na Mungu katika kuliombea Bunge hilo linaloendelea hivi sasa.

Alisema sasa Bunge lina mtikisiko mkubwa ambao unaoonekana kuvamiwa na nguvu ya shetani, na Watanzania kukosa imani juu ya malumbano hayo yanayochukua muda mwingi kupitisha kanuni ambazo zinategemewa kusaidia kupatikana Katiba iliyo bora kwa maslahi ya Watanzania wote.

“Suala la kutengeneza Katiba ni la kitaifa, hivyo kunahitajika hekima ya Kimungu ili kuwepo na utulivu utakaosababisha kutafakari jinsi wajumbe watakavyotoa maoni yao na hatimaye ikapatikana Katiba ambayo itatumika kwa miaka mingi ijayo,” alisema.

Alisema suala hilo litafanikiwa kama kutakuwa na maombi mazito kutoka kwa waumini mbalimbali na pia wanawake kwani bila hivyo kuna hatari ya kupata Katiba iliyochakachuliwa na shetani ambayo itaipeleka nchi mahali pabaya.

Awali akizungumza katika ibada hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Pwani, Mchungaji Ernest Kadiva aliwataka wanawake kutoka madhehebu mbalimbali ya dini kuendelea kuombea Bunge hilo la Katiba ili Watanzania waweze kupata Katiba inayotokana na Mungu.

Alisema bila maombi kuna hatari watanzania wakapata Katiba ambayo itakuwa na upungufu mkubwa.

“Kama katiba itakuwa na mapungufu itasababisha hata kizazi chetu kutoelewana na hatimaye kukawepo na vurugu ndani ya nchi,” alisema.

Pia alisema wanawake wanategemewa kwa kila jambo ndani ya jamii na hata kwa Taifa, hivyo ni jukumu lao kuliombea Bunge hilo ambalo hivi sasa lipo kwenye mchakato wa kupitisha kanuni na hatimaye Katiba.

“Ikiwa Taifa litapata Katiba isiyo salama kwa ajili ya nchi yetu, tutaweza kutengeneza chuki kwa watoto wetu ambao tunaamini Katiba inayotengenezwa leo itasaidia maadili kwa vijana ambao wanawake walikuwa wa kwanza katika kuwalea,” alisema mchungaji huyo.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: