NA FRANK KIBIKI, IRINGA
WAKAZI wa kijiji cha Mazombe, mkoani Iringa wanashukiliwa na jesho la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kukutwa na kidole cha binadamu kutokana na imani za kishirikina.
Kaim Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa, Wankyo Nyigesa alisema tukio hilo limetokea April mosi na kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Gibson Kasenegala (29) na Benson Mlasu (23).
Alisema watuhumiwa hao, wakiwa pamoja walikuwa wakimiliki koidole hicho ambacho hakijulikanani cha nani, kutokana na imani za kishirikina kwamba kinaweza kuwasaidia kupata mali.
“Tumewatia mbaroni na uchunguzi wetu unaendelea ili tujue nani alikatwa kidole, au kama kuna mtu aliuawa kisha kidole chake kikachukuliwa,” alisema Nyigesa.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi huo kukamilika.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / ANG'ANG'ANIWA NA JESHI LA POLISI KUFUATIA KUKUTWA NA KIDOLE CHA BINADAMU MKOANI IRINGA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment