BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 2 APATA SIFA KEDEKEDE BAADA YA KUPIGA SIMU 999 ILI MAMA YAKE APATIWE HUDUMA YA KUPELEKWA HOSPITALI KUFUATIA KUZIMIA GHAFLA NA KUDONDOKA CHINI UINGEREZA.

Riley Ward 
Mtoto mwenye umri wa miaka miwili nchini Uingereza Riley Ward amepokea sifa kedekede kwa kuokoa maisha ya mamake kwa kupiga nambari ya simu 999 baada ya mamake kuzimia.

Wahudumu wa afya katika kituo cha kupokea simu za dharura nchini Uingereza walisema kuwa walipokea simu ya mtoto mdogo aliyewambia ''Mama amelala''.
Wahudumu hao walifanikiwa kwenda nyumbani kwa mtoto huyo katika mtaa Leicestershire, na kumpa huduma ya kwanza mamake mtoto huyo na kisha kumpeleka hospitalini. 

Walimfanyia upasuaji wa dharura baada ya kupatikana na damu iliyokuwa imeganda kichwani huku akivuja damu nyingine kutoka katika kizazi chake. 


Sasa mtoto huyo Riley Ward amezawadiwa kwa kitendo chake cha ujasiri na wahudumu hao waliosema kuwa huyo ndiye mtoto mchanga kabisa kuwahi kupiga simu kituoni humo.
Mamake , Dana Henry, alimtaja mwanawe kama shujaa wake mdogo. 


Dana mwenye umri wa miaka 27 alisema kuwa alishtushwa sana na kitendo cha mtoto wake aliyekuwa na uwezo wa kupiga simu.
Pia alisema kuwa ameweza kuwafundisha watoto wake wadogo namna ya kupiga simu ya dharura ikiwa yeye na mumewe hawahisi vizuri.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: