SHIRIKA LA NDEGE LINALOTOA HUDUMA KWA BEI RAHISI YASAFIRISHA ABIRIA ZAIDI YA 450,000 NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA KWA WIKI 16 TU.
Kampuni ya Ndege inayotoa huduma kwa bei rahisi ya Fast Jet mpaka sasa imefanikiwa kusafirisha jumla ya abiria 500,000 katika safari zake za ndani na nje ya nchi.
Afisa uhusiano wa Fast Jet Lucy Mbogoro amesema kampuni hiyo imefanikiwa kusafirisha kiasi hicho cha abiria hao kwa kipindi cha miezi 16 ambayo ni sawa na abiria 31,250 kila mwezi, Fast jet kwa sasa imeongeza pia safari za Mwanza ambapo imekua ikienda hadi usiku.
Fast Jet pia inaenda Lusaka na South Africa abiria aliyefikisha idadi ya kuwa abiria wa Laki Tano alizawadiwa chakula cha usiku kwenye hotel ya Hyatt Hotel.
0 comments:
Post a Comment