ENEO LA TUKIO LA AJALI YA UDONGO KUWAFUKIA WATU 2000 NCHINI AFGHANISTA.
Juhudi za uokoji zinaendelea siku ya pili Kaskazini
mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao elfu mbili wanasadikiwa
kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa
wa Badakhshan.
Miili ya watu wapata 350 imepatikana hapo jana katika maporomoko ya ardhi kazkazini mashariki mwa taifa hilo na hakuna mtu yoyote aliyepatikana akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema karibu watu 4000 hawana makazi.
Waokoaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka manusura.
Mwandishi wa BBC mjini kabul anasema kuwa eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yenye umaskini mkubwa na katika taifa maskini duniani na huenda ikachukua majuma kadhaa kabla ya serikali kubaini ukubwa wa janga hilo.BBC
0 comments:
Post a Comment