BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

IVORY COAST, COLOMBIA NA ITALY ZAONDOKA NA USHINDI DHIDI YA WAPINZANI WAO KATIKA MICHEZO YA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014.

491712799ML00219_Cote_D_IvoEngland ilikipiga na Italy kwenye mchezo ulioanza saa 7 ya usiku kwa saa za Afrika mashariki.


Matokeo ya mchezo huo yalikuwa ushindi wa 2-1 kwa Italy, Mario Balotelli akiibuka shujaa kwa goli la ushindi.

Marchisio alianza kuipatia goli la kuongoza Italy kwenye dakika ya 35, kabla ya Sturridge kusawazisha dakika 2 baadae na mchezo kwenda mapumziko sare.

Kipindi cha pili Super Mario Balotelli akaifungia Italy goli la ushindi.

Mchezo huo ambao ulianza majira ya saa 10 usiku, umeisha kwa Ivory Coast kuitoa kimasomaso Afrika kwa kuwa timu ya kwanza kushinda kwenye michuano ya mwaka huu baada ya kuitungua Japan 2-1.

Magoli ya Ivory Coast yamefungwa na Wilfred Bony na Gervinho – Keisuke Honda aliifungia Japan goli la kufutia machozi.

Mchezo mwingine kwenye kundi hilo ulichezwa mapema kiasi saa mbili usiku kati ya Colombia dhidi Ugiriki.

Matokeo yalikuwa 3-0 kwa ushindi wa Colombia ambayo ilimkosa staa wao Radamel Falcao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: