BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MABINGWA WATETEZI KOMBE LA DUNIA HISPANIA YAKIONA CHA MTEMA MOTO KUTOKA KWA UHOLANZI, YAIGALAGAZA KWA KUITUNGUA BAO 5-1 KATIKA MCHEZO WAO WA UFUNGUZI WA KOMBE HILO NCHINI BRAZIL 2014.

Stefan de Vrij (kushoto) akiifungia Uholanzi bao la tatu.
Mharibifu: Robin van Persie akimkumbatia Arjen Robben baada ya kufanya makubwa usiku huu.
MABINGWA watetezi wa kombe la dunia, Hispania, wamechapwa kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 5-1 jana usiku kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa kombe la dunia nchini Brazil dhidi ya makamu bingwa wa michuano hiyo, timu ya taifa ya Uholanzi. 


Mechi hiyo ilijirudia kama ile ya fainali ya mwaka 2010 nchini Afrika kusini ambapo Hispania walishinda bao 1-0, lakini Uholanzi wamelipa kisasi kwa kutoa `mvua ya kutosha`. 


Miaka mitano iliyopita, Hispania walipoteza mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Switzerland, lakini kipigo kile huwezi kukifananisha na cha usiku wa jana. 


Kocha wa Hispania Vicente del Bosque atajiuliza kwanini timu ilipotea katika mazingira ya kushinda wakati waliongoza kwa muda mrefu. 


Nini kitawaamusha Hispania ambao walipoteana, wakashindwa kujiamini , yaani wakakosa nidhamu ya mchezo baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-1. 


Kipindi cha pili, mabingwa hao watetezi walikubali kila kitu na kuwaacha Uholanzi wakicheza mpira na kufunga magoli mengi, hivyo kuanza kufirika kama wanaweza kuwa mabingwa ingawa ndio kwanza ngoma mbichi.

Ndosi hiyo!: Robin van Persie akifunga goli kwa kupiga kichwa matata na kuisawazishia Uholanzi.
Kosa kubwa la mlinda mlango: Van Persie akimpoka Iker Casillas mpira na kufunga bao la nne.
Haamini: Casillas akitafakari baada ya kufungisha bao la nne, huku wachezaji wa Uholanzi wakishingilia bao hilo la Van Persie


Vikosi na viwango vya wachezaji katika mchezo wa leo kwa mujibu wa Joe Callaghan ambaye yupo mjini Sao Paulo. Alama zilizotumika ni 10.


Kikosi cha Hispania: Casillas 5, Azpilicueta 6.5, Sergio Ramos 5.5, Pique 5.5, Jordi Alba 7, Alonso 7.5 (Pedro 63), Xavi 7, Busquets 6, Silva 7.5, Diego Costa 7 (Torres 62), Iniesta 7. 


Wachezaji wa Akiba: De Gea, Albiol, Javi Martinez, Juanfran, Villa, Fabregas, Mata, Koke, Cazorla, Reina.


Kikosi cha Uholanzi: Cillessen 7, Janmaat 6, Vlaar 7.5, De Vrij 7, Martins Indi 6.5, Blind 7, de Guzman 6, Sneijder 6, De Jong 6.5, Van Persie 8, Robben 8. 


Wachezaji wa akiba: Vorm, Verhaegh, Veltman, Kongolo, Kuyt, Clasie, Lens, Fer, Huntelaar, Wijnaldum, Depay, Krul.
Mwamuzi: Nicola Rizzoli (Italia) 


Mchezaji bora wa mechi: Robin van Persie na Arjen Robben
Mabao yote ya Uholanzi yalikuwa ya ajabu. Yote yalitengenezwa kwa pasi murua kutoka wingi ya kushoto kutokea kwa Daley Blind na pasi zilimaliziwa kwa ufundi tofauti na wachezaji Robin van Persie na Arjen Robben. 


Magoli manne yalitokana na makosa ya mlinda mlango Iker Casillas. Kuelekea mechi ijayo itakayochezwa wiki ijayo ambayo Hispania wanahitaji ushindi- kuna hoja kuwa kipa wa Manchester United, David de Gea anaweza kumbadili mlinda mlango huyo mkubwa wa Hispania.

Bao la tano: Robben (kushoto) akiifungia Uholanzi bao la tano.

Hapa anageuzwa: Arjen Robben akimpiga chenga Gerard Pique Sergio Ramos alishindwa kumzuia Robben, aliyepiga mpira na mguu wake wa kushoto na kuandika bao. Iker Casillas (kulia) alipelekwa sokoni Louis van Gaal akimpa tano Van Persie baada ya kufunga bao kusawazisha. Fungeni midomo: Diego Costa akiwanyooshea kidole mashabiki wa Salvador ambao walimzomea dakika zote alipokuwa uwanjani.
Costa aliangushwa na Stefan de Vrij na mwamuzi kuamuru mkwaju wa penati
Xabi Alonso alifunga penati hiyo
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: