BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UJERUMANI YATOA ONYO KUNDI G BAADA YA KUIGALAGAZA URENO YA RONALDO KWA KUITANDIKA BAO 4-0 KOMBE LA DUNIA BRAZIL HUKU UTABIRI WA NGAMIA UKIGONGA MWAMBA.


Mshambuliaji wa Ureno Christiano Ronaldo akikabiliana na beki wa Ujerumani.

Michuano ya kombe la dunia inayofanyika nchini Brazil imezidi kushika hatamu, kwa michezo mitatu kupigwa usiku wa kuamkia leo.
Mechi ya kwanza ilishuhudia Ujerumani ikiwaadhibu Ureno kwa kipigo cha magoli 4-0.

Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Thomas Muller ambaye aliandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye michuano hii kufunga hat trick, huku beki Matt Hummels akikamilisha idadi ya magoli 4.

Ushindi huo wa Ujerumani umekwenda kinyume na utabiri wa Ngamia ‘Shakeen’ ambaye aliitabiria Ureno ushindi.

Mchezo wa pili jana ulihusisha timu na Nigeria dhidi ya Iran ambao uliisha kwa sare tasa.

Wawikilishi wengine wa Afrika, Ghana walikuwa wakikutana na USA, na matokeo – Ghana walipoteza mchezo huo kwa kufungwa 2-1.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: