BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAARIFA RASMI !!: MAHAKAMA NCHINI UGANDA YATENGUA SHERIA YA USHOGA.


Wanaume wanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja Uganda

Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.

Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya Magharibi yalilazimika kuingilia kati.

Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada na kwa hivyo ni kinyume na sheria.

Baadhi ya waandamanaji waliounga mkono serikali kwa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja.
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa Uganda , lakini sheria hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati huu hata kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia moja.

Mataifa kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: