BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MALAYSIA KUISAKA UPYA NDEGE YAKE YA MH-370 ILIYOPTEA MIEZI SABA ILIYOPITA KATIKA BAHARI YA HINDI.


Malaysia imeanza awamu nyingine ya kuisaka ndege yake iliyopotea MH-370 kusini mwa bahari ya Hindi ikiwa ni takribani miezi saba tangu kutoweka kwa ndege hiyo. Meli iliyofungwa vifaa maalumu vinavyotumia teknolojia ya Sonar.

Hata hivyo meli hiyo ikiwa na vifaa hivyo imewasili katika eneo la pembezoni kabisa mwa Bahari ya Hindi kilomita 18,000 magharibi mwa Australia,

Utafutaji wa ndege hiyoilisitishwa kwa muda kwa kipindi cha miezi minne ili kutoa nafasi uchunguzi zaidi wa ramani kuhusiana na kupotea kwa ndege hiyo.

Ndege hiyo ilipotea mwezi march mwaka huu wakati iliporuka kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: