BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA MAZISHI YA MABAKI MIILI YA ABIRIA WALIOUNGUA MOTO, AJALI BASI LA NGANGA NA FUSO RUAHA WILAYA YA KILOSA MOROGORO.

Kijiko cha kampuni ya sukari Kilombero kikifukia kaburi la pamoja la miili ya watu 15 walioteketea kwa moto katika ajali ya Basi la Nganga na Fuso iliyotokea Iyovi, Ruaha Mbuyuni. Mazishi hayo yalifanyika jana katika Kijiji Nyavisi Ruaha, wilayani Kilosa, Morogoro. Picha na Juma Mtanda. 



 Sehemu ya umati wa ndugu, jamaa na marefiki wakishuhudia tukio la kuzikwa kwa wapendwa wao
Ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliofariki katika ajali hiyo wakiwa wameba mabaki ya miili baada ya kushushwa kutoka kwenye gari tayari kwa mazishi.

Hapa ikihifadhi katika kaburi la pamoja kabla ya kijiko cha kampuni kiwanda cha sukari Kilombero kuanza kufukia udongo wakati wa mazishi hayo.

Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro (RTO) Boniface Mbao wa aliyeinamisha fimbo chini akiwa na safu ya maafisa wengine wakati wa tukio la kuzika mabaki ya miili ya marehemu hao.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa John Henjowele akizungumza jambo na mamia ya watu waliohudhiria mazisha hayo.
Mwoombolezaji akilia huku akiwa ameshikilia picha ya mmoja wa watu 19 waliofariki katika ajali hiyo wakati wa mazisha hayo
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Zitto Kabwe na viongozi wengine wakiwa wenye majonzi wakati wa mazishi hayo, Zitto na wenzake walitarajia kufanya mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ruaha lakini mkutano huo haukuweza kufanyika kutokana na shughuli ya mazishi hayo.
Huyu ni mmoja wa waombolezaji ambaye alizimia baada ya kuona mifuko iliyohifadhiwa mabaki ya miili hiyo.

 Sehemu ya ndugu, jamaa na marafiki waliofiwa na ndugu zao wakiwa wenye majonzi
 Wakiomba dua zilizokuwa zinatolewa na viongozi wa dini mbalimbali




Mpiga Picha wa ITV, Sifuni Mshana akiwa katika harakati za kuchukua picha eneo la chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya St Kizito Mikumi Morogoro.

Na Hamida Shariff na Juma Mtanda, Mwananch
i
Morogoro. Maiti 15 kati ya 19 za watu waliopoteza maisha katika ajali ya Basi la Nganga Express na lori iliyotokea juzi eneo la Iyovi, Milima ya Udzungwa mkoani Morogoro wamezikwa jana katika kaburi la pamoja eneo la Msamvu Kijiji cha Nyanvisi kata ya Ruaha wilaya ya Kilosa mkoani hapa.


Simanzi na vilio vilitawala katika eneo hilo wakati miili ya watu hao ilipofikishwa hapo saa saba mchana kabla ya mazishi hayo kuanza ya saa 8.30 mchana.


Viongozi wa dini zote walifanya misa za kuwaombea marehemu hao waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambayo baada ya kutokea, basi na lori hilo aina ya Fuso yaliteketea kwa moto na abiria waliokuwamo.


Akizungumza katika mazishi hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, John Henjewele alisema tukio hilo ni la kusikitisha na la tofauti ambalo limeitia simanzi nchi nzima. 

“Ni tukio la nadra sana, lakini pia naweza kusema ni la kizembe kwa sababu tayari tumejua chanzo cha ajali hiyo,” alisema. Henjewele alisema wamepata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu madereva wanaoendesha magari ovyo.


“Nawapongeza vijana wa eneo hili kwa kusaidia kutoa miili kwenye magari licha ya kuwa moto ulikuwa unawaka,” alisema Henjewele katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa pia na Kiongozi wa ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe.

Kati ya maiti hizo 19 ni maiti wanne tu ndiyo waliotambuliwa na ndugu zao kisha kuzikwa katika utaratibu wa kawaida na wengine 15 walizamika kuzikwa kaburi moja.
Miili ya abiria wengine sita, imetambuliwa na ndugu zao ilikohifadhiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito, Mikumi Wilaya ya Kilosa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo aliwataja marehemu waliotambuliwa katika ajali hiyo kuwa ni Hadija Legembo (35), mkazi wa Kilombero; Lidya Ndongwe (16), mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Mtakatifu Francis Mbeya na Ester Mgimba (30), mkazi wa Njombe. 
Wengine ni Nelson Patrick, mtoto wa miaka miwili mkazi wa Njombe, Marietha Ponsiano (19) mkazi wa Kilombero, Mengo Njagaje (30), mkazi wa Mbeya. Kamanda Paulo aliwataja majeruhi 10 wa ajali hiyo kuwa ni Majaliwa Elisha (21), mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya St Mary Mbeya; Linda Jonathan (26), mkazi wa Mbeya, Rose Seth (18), mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Sanje Kilombero na Elias Augustino (36), mkazi wa Kilombero. 
Majeruhi wengine ni Batista Emmanuel (44), mkazi wa Mbeya, Abubakar Athumani (36), mkazi wa Ruaha, Emmanuel Omarino (18), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Konsolata Iringa; Teresia Kusila (25), mkazi wa Ruaha, Shafii Mussa (25), mkazi wa Kilombero na Anyindwile Elia (30), kondakta wa Basi la Nganga Express.


Chanzo cha ajali
Kamanda Paulo alisema basi hilo lilipata ajali likiwa linatokea Kilombero kwenda Mbeya likiwa na abiria 27.

Alisema lilikuwa likiendeshwa na Batista Emanuel (44) na lilipofika Iyovi, kilomita 75, kutoka Mji wa Mikumi, dereva huyo alihama na kwenda upande wa kulia zaidi mwa barabara na kugongana uso kwa uso na Fuso ambalo dereva wake bado hajafahamika.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: