BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VURUGU BURUNDI: MTU MMOJA APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA HUKU RAIS NKURUNZIA AKISAKATA KANDANDA BUJUMBURA.


 

RAIS PierreNkurunziza akijiburudisha kwa kusakata kandanda mjini Bujumbura Burundi.

Habari kutoka Burundi zinasema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Bujumbura.

Mtu huyo alikuwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa awamu ya tatu.

Walioshuhudia wanasema kuwa polisi walimpiga mwandamanaji huyo risasi mgongoni wakiwa katika eneo la Musaga linalotazamwa kama ngome ya upinzani.

Waandamanaji walijaribu kufika katikati mwa jiji la Bujumbura lakini walitimuliwa kwa mabomu ya moshi wa kutoa machozi.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewaomba zaidi ya raia laki moja na hamsini waliokimbia ghasia nchini humo katika majuma kadhaa yaliyopita, warejee nyumbani.

Katika hotuba kwenye runinga ya taifa, amesema kuwa asilimia tisini na tisa nukta tisa ya Burundi ina amani.

Anasema kuwa hakuna mtu yeyote anayetaka kufufua taharuki ya kikabila.

Muda mchache baadaye rais Nkurunziza alionekana akicheza mpira na maswahiba wake wa karibu licha ya maaandamano yanayoendelea mjini Bujumbura.

Kumekuwa na hali ya taharuki mjini Bujumbura haswa kutokea jumatano iliyopita baada ya jaribio la mapinduzi dhidi ya rais Nkurunziza

Rais Nkurunziza amehitimu kama kocha wa kandanda.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: