BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUTANA NA BIBI KIZEE (85) MTAALAMU WA KUIBA HELENI KATIKA MADUKA YA VITU VYA THAMANI KAZI ALIOIFANYA KWA ZAIDI YA MIAKA 60 SASA.


Doris Payne, anatuhumiwa kwa wizi wa herini ya thamani ya dola 690.

Bibi kizee mmoja mwenye umri wa miaka 85 raia wa Marekani na ambaye amekuwa akiiba vito vya thamani kwa zaidi ya miaka 60 amehukumiwa tena kwa kosa la wizi.

Doris Payne, anatuhumiwa kwa wizi wa herini ya thamani ya dola 690, kutoka katika duka moja la uuzaji wa vitu vya thamani la Saks katika kiunga kimoja mjini Atlanta-Marekani.

Wakili wake anatafuta namna ataachiwa huru kwa sababu ya kudorora kwa afya yake.

Payne, ambaye maisha yake ya wizi yaliwekwa katika filamu mwaka 2013, amewahi kufungwa jela mara kadhaa kwa makosa mengi tu ya wizi na uhalifu.

Wakuu nchini Marekani wanasema kuwa, ametumia majina 22 ya bandia tangu alipoiba almasi kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 23, na akaweza kukwepa kutiwa mbaroni.

Muungano wa Walinzi wa vitu vya thamani JSA, kampuni moja kubwa ya kibiashara, ilituma tahadhari kwa maduka yote yanayouza bidhaa na mapambo ya thamani kujihadhari na mwizi huyo sugu mapema miaka ya 70.

Rais wa kampuni hiyo kubwa alitaja tabia ya bi kizee huyo kama wizi au uhalifu wa aina yake.

Aidha anastaajabu kuwa angali anaiiba hata akiwa na umri huo mkubwa.

Akihojiwa na shirika la habari la Associated Press mwaka 2005, akiwa jela, bibi huyo Payne, alisema kuwa haibi kwa sababu ya pesa; ila yeye hujikuta tu akiiba na haoni kama ataacha tabia hiyo, labda baada ya kufa.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: