Akizungumza na wakazi wa Ileje, Mbene alisema ushindi wa kura 27,583 aliopewa na wana Ileje dhidi ya Emmanuel Mbuba wa NCCR Mageuzi aliyepata kura 14,578 atahakikisha anawapa wananchi hao kupitia ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakalibi.
“Awali ya yote niwashukuru wana Ileje kwa kuonesha imani kubwa kwangu, madiwani na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Jonh Magufuli. Wana Ileje wametupa kura za kishindo nami ninawahaidi sitawaangusha katika utekelezaji wa ahadi nilizozitoa kwenu wakati wa kampeni,” alisema Mbene.
Mbunge huyo mteule alisema kuwa, kipaumbele chake cha kwanza kitakuwa mindombinu ya barabara na kuwajengea uwezo wajasiriamali ili kuzalisha bidhaa bora ikiwemo kuongeza thamani na mauzo.
Mbene alisema, hatua hiyo itasaidia kuondoa umaskini wa kipato na msisitizo utakuwa kwenye ufugaji wa samaki, kuku, nyuki na mifugo ya kisasa.
Pia alisema, kilimo nacho atakipa kipaumbele hususani cha alizeti,
kunde, choroko, dengu, mbaazi, soya , karanga zikiwemo njugu mawe kwa wingi kama mazao ya biashara.
“Nitahakikisha pia kilimo cha nafaka ambacho kitahusisha mahidi,
mpunga, ulezi , mtama na kilimo cha matunda aina mbalimbali yakiwemo mananasi , maembe, maparachichi, mapera zikiwemo mbogamboga ili kuwainua wana Ileje kupitia kilimo chenye tija,” alisema Mbene.
Mbali na hayo alisema, kwa kushirikiana na wananchi ataibua vyanzo vya asili ambavyo ni vivutio vya watalii wilayani Ileje ili viweze kuwavutia watalii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Pia alisema, atahakikisha anashirikiana na wananchi ili kuhakikisha
wanatatua kero mbalimbali katika sekta ya elimu, afya na miundombinu hatua ambayo itasaidia kuinua vipato vyao, jimbo na taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment