BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ALIKOCHIMBULIWA NAIBU SPIKA WA BUNGE, ALIANZA KIKWETE KISHA RAIS MAGUFULI

Naibu Spika wa BungeDk Tulia Ackson Mwansasu.

By Louis Kolumbia, Mwananchi Digital
Dar es Salaam.
Wabunge 250 wamepiga kura za ndiyo kwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Viti Maalumu, vya kuteuliwa na rais, Dk Tulia Ackson Mwansasu na kumchagua kuwa Naibu Spika wa Bunge la kumi na moja.

Akitangaza matokeo hayo Bungeni mjini Dodoma leo, Dk. Thomas Kashilillah amesema mgombea toka Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya amepata kura 101 sawa na asilimia 28.8 ya kura zote zilizopigwa.

Amesema ushindi alioupata Dk Tulia ni sawa na asilimia 71.2 ya kura zote zilizopigwa na kwamba hakuna kura iliyoharibika.

Alisema idadi ya wabunge wote katika Bunge hilo ni 394 huku 364 ndiyo waliojisajili na kushiriki uchaguzi huo. Wabunge 189 ndiyo wenye uwezo wa kufanya uamuzi (akidi). Hata hivyo, waliopiga kura ni 351.

Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson  akila 
Dk Tulia amezaliwa Novemba 23, 1976 eneo la Bulyaga, wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Alipata elimu ya awali katika Shule ya Mabonde wilayani Tukuyu kati ya mwaka 1984 na 1990 kabla ya kujiunga na shule za Lolera na Zanaki kwa elimu ya sekondari kati ya mwaka 1991 na 1997.

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1998 kwa Shahada ya kwanza ya Sheria kabla ya kurejea tena Chuoni hapo mwaka 2001 na kufanikiwa kutunukiwa Shahada ya pili, mwaka 2003.

Mwaka 2005-2007 alijiunga na Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini kwa digrii ya udaktari wa filosofia katika sheria kabla ya kurejea nyumbani na kuhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Februari 2014 Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete alimteua kuwa mbunge wa Bunge Maalum la Katiba (BMLK) kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuuwa Serikali Septemba 9, mwaka huu.

Alichukua fomu kuwania Uspika kupitia CCM kabla ya kujitoa dakika za lala salama kisha akateuliwa na Rais Magufuli luwa mbunge wa viti maalumu kwa mujibu wa madaraka yake ya urais.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: