BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DAKTARI AGOMA KUTOA HUDUMA KWA MTOTO WA MIEZI SITA BUKOMBE

Daktari akitekeleza majukumu yake.

Bukombe. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, James Ihunyo ameunda kamati ya watu watatu inayoongozwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya, Dk Maja Sosome kuchunguza tuhuma zinazomkabili mganga aliyekuwa zamu usiku wa Novemba 22, mwaka huu kugoma kumhudumia mtoto mwenye umri wa miezi sita.

Licha ya kuundwa kwa kamati hiyo, Ihunyo amemsimamisha kazi mganga huyo, Dk Johannes Mkobwe ili kupisha uchunguzi.

Akizungumza kwa simu juzi, Ihunyo alisema kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma, amemwandikia daktari huyo barua ya kumsimamisha ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili, baada ya ripoti ya kamati atatoa uamuzi.

Ihunyo aliwataja wengine wanaounda kamati hiyo kuwa ni Ofisa Muuguzi Mkuu wa Wilaya, Pendo Mhoja na Ofisa Utumishi, Baraka Enock ambao watafanya kazi kwa siku saba, ikiwamo kuwahoji wazazi wa mtoto huyo.

Inadaiwa Novemba 22 saa 10:00 alfajiri, Jeremia Manyama (41) na mkewe, Sarah Reuben walimfikisha mtoto wao, Johnson katika hospitali ya wilaya akiwa anatapika na kuharisha, lakini daktari huyo alikataa kumhudumia kwa madai kuwa alikuwa amechoka.

Baada ya kugoma kuwahudumia, wazazi hao walimpigia simu mkuu wa wilaya hiyo, Amani Mwenegoha na alifika hospitalini hapo kisha kumpigia Sosome ili afike kumhudumia mtoto huyo.

Kutokana na jambo hilo, Mwenegoha aliagiza Mkobwe asimamishwe kazi.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: