BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JESHI LA POLISI LAMTUNISHIA MISULI WAZIRI WAKUU WASTAAFU EDWARD LOWASSA NA MWENZAKE FREDERICK SUMAYE MWANZA


Viongozi wa Chadema wakiondoka kwenye Hospitali ya Bugando jijini Mwanza jana, baada ya kushindwa kuchukua mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Geita, Alphonce Mawazo. Picha na Michael Jamson

Mwanza.
Shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Aphonce Mawazo aliyeuawa wiki iliyopita iko katika sintofahamu baada ya chama hicho kudai kuzuiwa na polisi kuuchukua mwili huo katika Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC) ulikohifadhiwa.

Viongozi wa kitaifa wa Ukawa na Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe akiambatana na aliyekuwa mgombea urais, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, wakurugenzi wa Chadema na wabunge wa upinzani waliwasili jijini Mwanza, lakini hadi tunakwenda mitamboni hawakuwa wamechukua mwili huo.

Taarifa ya Chadema iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari, Tumaini Makene baadaye jioni ilisema vikao vilikuwa vinaendelea na kuwa taarifa za kina zingetolewa baadaye.

Viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa, walifika BMC jana saa 5.35 asubuhi kuuchukua mwili, lakini hawakufanikiwa na wakaondoka wakieleza kuwa wanakwenda kufanya mazungumzo kujadili suala hilo.

Makene alisema: “Baada ya viongozi hao kuwasili na kupewa taarifa za awali kuhusu maandalizi ya ratiba ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Kamanda Mawazo, wamesikitishwa sana na kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuzuia shughuli hiyo kufanyika jijini humo.”

Akizungumzia kwa nini Mawazo aagwe Mwanza na baadaye Geita, Makene alisema mbali ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita, pia alikuwa kiongozi wa Kanda ya Ziwa ambayo inajumuisha mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita.

Msimamo wa polisi
Hata hivyo, polisi walikanusha madai ya kuwazuia Chadema kuchukua mwili huo lakini wakasisitiza kuwa wamezuia shughuli za kuaga mwili huo zilizopangwa kufanyika katika ofisi za Kanda ya Ziwa za chama hicho.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo alisema wamefanya mazungumzo na baba mdogo wa marehemu, Mchungaji Charles Lukiko kuwa mwili huo watauchukua kesho (leo) na kwenda kuzika mkoani Geita.

“Sisi hatujawazuia Chadema kuchukua mwili wa Mawazo, ila wao wameingiza mambo ya kisiasa, tunachosema polisi ni kwamba hatutaki shughuli za kuaga mwili huo zifanyike mkoani hapa, wala mkusanyiko wa aina yoyote.”

Mkumbo alisema wamezuia mikusanyiko ya aina yoyote kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Baadaye Mchungaji Lukiko alisema familia itauchukua mwili wa marehemu kati ya leo na kesho kutoka Bugando na kuupeleka moja kwa moja Geita kwa ajili ya mazishi.

“Bado kuna mvutano, Chadema wapo kwenye vikao vyao, wanataka kuuaga mwili wa mwenzao, lakini na sisi kama familia tunatarajia kati ya Jumapili au Jumatatu tutauchukua. Kwa sasa siwezi kusema zaidi ya hapo,” alisema Mchungaji Lukiko.

Shughuli hizo za kuaga mwili zilitarajiwa kufanyika jana kwenye Viwanja vya Furahisha au Ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa.

Awali, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Kigaila Benson alisema: “Tunashangaa polisi kutuzia kuuga mwili wa Mawazo, tulikubaliana kwamba mwili utaagwa katika ofisi za Kanda, lakini wametugeuka na kutuzuia kufanya hivyo utadhani sisi ni wahalifu.

“Mawazo hajafa kwa kipindupindu, wala hatuendi kula chakula tunataka tumuage ndugu yetu, wanavyotumia nguvu kubwa sijui inaashiria kitu gani, ni jambo la kusikitisha kwani angekuwa kafa mtu wa upande wa pili angeagwa na ulinzi angepewa.”

Mkurugenzi wa Chadema Kanda ya Ziwa, Peter Makere alisema Chadema ni jeshi kubwa zaidi na kwamba kwa vyovyote lazima mwili wa mwenzao uagwe kabla ya kwenda kuzikwa Geita.

Ulinzi mkali kila kona

Jana, Jiji la Mwanza lilipambwa na askari polisi waliyokuwa na sare na waliokuwa wamevalia kiraia kila kona baadhi yao wakiwa wamebeba silaha za moto na wengine mabomu ya machozi na wengine wakiwa na mbwa.

Polisi walitanda katika Barabara Kuu inayoingia kutoka mikoa kati, Hospitali ya Rufaa Bugando na kwenye ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa zilizopo kona ya Bwiru.

Mawazo aliuawa Novemba 14 baada ya kuvamiwa na kundi la watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM na tayari watu watano wamefikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: