MKUU WA MKOA WA MBEYA AWAONGOZA WANANCHI KUFANYA USAFI KATIKA MASOKO MANNE KWA UTII BILA SHURUTI.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Gabriel Makalla amewaongoza wakazi wa jiji la Mbeya kufanya usafi katika masoko ya Soweto, SIDO na Kabwe.
Akizungumza mara baada ya kushiriki kufanya usafari, Makalla amnewataka wananchi wa Mbeya kuweka miji yote na jiji la Mbeya katika hali ya usafi ili kulingana na hadhi ya jiji.
Makalla alisema kuwa wananchi wanapaswa kujenga tabia ya kufanya usafi kwa kuanzia ngazi ya kaya, kitongoji, mtaa, na kwenye masoko yote.
"Naagiza uongozi wa jiji kuzoa takataka ngumu zote kwa wakati na kuongeza magari ya kuzoa takataka ili isiwe chanzo cha kurundikana takangumu katika maeneo ya kuhidhia taka kwa muda".alisema Makalla.
Aliongeza kwa kusema amewashukuru wananchi kwa moyo wa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi na waendelee kujitokeza mara kwa mara kufanya usafi katika siku za usoni ili jiji hilo liendelea kuwa safi na mandhari ya kuvutia.
0 comments:
Post a Comment