BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DIWANI WA CCM ATIMULIWA KWA NGUVU KWENYE MKUTANO WA MTAA NA WANANCHI WENYE HASIRA NAYE MOROGORO.

Diwani wa kata ya Mindu, Hamis Msasa akizongwa na baadhi ya wanaume wenye jazba katika mtaa wa Lugala wakati wa kumtimua katika mkutano wa hadhara wa kuunda wanakamati ya wajumbe 10 ili kwenda Dodoma kupeleka kero mbalimbali kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa uliofanyika jana kwenye shule ya msingi Lugala Manispaa ya Morogoro.PICHA/JUMA MTANDA

Juma Mtanda, Morogoro.

Diwani wa kata ya Mindu amefukuzwa kwa nguvu katika mkutano wa hadhara wa kuunda kamati ya watu 10 ya kwenda Dodoma kupeleka kero kwa waziri mkuu Kassimu Majaliwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakazi wa mtaa wa Lugala kudai, uongozi wa halmashauri ya Manispaa umeshindwa kuwasaidia kupata ufumbuzi wa jengo la shule lililojengwa chini ya kiwango na kuanguka huku wanafunzi 85 wakikosa masomo kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja mkoani Morogoro.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Lugala, Sanga Mgulago pamoja na Afisa Mtendaji wa mtaa huo, Makame Kai kwa moja walijaribu kuzuia wananchi wasimuondoe diwani huyo lakini walizidiwa nguvu na kumuondoa kinguvu kutoka kwenye kiti alichokuwa ameketi katika meza kuu ya viongozi.


Wakizungumza kwa jazba muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo, majira ya saa 10 jioni eneo la shule ya msingi Lugala wananchi hao walianza kwa kumweleza Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Sanga Mkulago kumtimua diwani wao, Hamis Msasa kwa madai kuwa amekuwa msaliti katika vikao vya maendeleo na amekuwa sio msaada tangu achaguliwe nafasi hiyo.

Joseph Zambi na Mbena Chunda walisema kuwa diwani huyo amekuwa msaliti na ameshindwa kuchukua kero za mtaa huo ili ziweze kutatuliwa na halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ikiwemo wanafunzi 85 wa darasa la kwanza na pili kukosa masomo kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa tangu jengo la madarasa mawili lianguke.

“Tuna kero nyingi na zimeshindwa kutatuliwa na viongozi wetu lakini kubwa zaidi ni jengo lililojengwa chini ya kiwango kuanguka na wanafunzi wetu wamekuwa wakishinda nyumba na kukosa masomo kwa kipindi cha mwezi moja.”alisema Zambi.

Kwa upande wa Chunda alieleza kuwa wanafunzi hao walikuwa wanakabiliwa na changamoto za kutembea umbali mrefu kwenda shule za jirani lakini baada ya kukamilika kwa vyumba vya madarasa hayo ilionekana kusaidia kuondokana na kero ya watoto wao kunusurika kusombwa na maji katika mto Ngerengere na mito ya msimu hasa katika kipindi cha masika ambayo imekuwa ikifulika maji na kuhatarisha usalama wa wakazi hao.

Kabla ya kuondoka kwa diwani huyo, Hamis Msasa alisikika akisema kwa sauti ya chini kuwa hakuna haja ya kumsuma na kumuondoa kwa nguvu na badala yake wamuache ili aondoke mwenyewe bila kushurutishwa.

“Niachezi naondoka mwenyewe kwa hiyari yangu na hakuna haja ya kunishika na sipendi mnisukume”.alisema Msasa.

Mkutano huo uliokuwa chini ya Afisa wa serikali ya mtaa Lugala, Makame Kai aliwaeleza wakazi hao lengo la mkutano huo kuwa ni kuunda wajumbe wa kamati ya watu 10 akiwemo mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo pamoja na yeye kwenda kwa waziri mkuu Dodoma kupeleka kero zinazowakabili.

“Kwa maelezo yenu mmenitaka niitishe mkutano wa kuunda kamati ya wajumbe 10 ili kwenda kupeleka kero zenu kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa bungeni Dodoma hilo kwa upande wangu sina tatizo nitasimamia na nitawaongoza.”alisema Kai.

Jengo la shule ya msingi Lugala ilianguka April 4 mwaka huu baada ya kunyesha mvua iliyoambatana na upepo mkali na kuezua paa na kuangusha chini mabati na ukuta hali iliyopelekea wanafunzi wa darasa la kwanza pili 18 na 67 wa darasa la kwanza kukosa masomo hadi sasa.CHANZO/MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: