BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JE WAJUA LUNDO LA SABABU ZA CHANZO CHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME ?.

 
Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo kubwa ambalo endapo halitatafutiwa ufumbuzi na mhusika linaweza kuyaathiri maisha yake kwa kiasi kikubwa sana. 

Mwanaume mmoja kati ya watatu wana matatizo ya nguvu za kiume, hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. 

Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini na jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama mhusika atazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. 


Mwanaume anayekabiliwa na tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume huonyesha dalili zifuatazo:-

1. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake barabara na kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali ) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume anaye kabiliwa na tatizo hilo uume wake hata ukisimama hubakia kuwa legelege na huweza kusinyaa wakati wowote. 


Tatizo hilo ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume, mishipa ya uume ndio inayoufanya uume usimame barabara na mishipa hiyo inapokuwa imelegea, uume hauwezi kusimama barabara hata iweje.
 

2. Kukosa hamu ya tendo la ndoa, Hapa mwanaume anakuwa hana uwezo wa kutamani kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa faragha na mke wake hivyo tatizo hilo kwa kiasi kikubwa husababishwa na msongo wa mawazo.

3. Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara moja, mwanaume huyo akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakuwa hana tena uwezo wa kurudia mshindo mwingine na hali hiyo husababishwa na kutokuwa na msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya kwenye uume. 



4.Mwanaume mwenye tatizo hilo hufika kileleni mapema na kutokuwa na uwezo wa kusimamisha kabisa hali hiyo hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume, linapokuwa limekomaa. 


Na wakati mwingine, hali hiyo hutokea pindi vyanzo zaidi ya kimoja vya tatizo la kiume vinapo kuwa vimejitokeza kwa mtu mmoja. 

6. Uume kusinyaa na kurudi ndani, hapo uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani na uume huo unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa.

Kwa ufupi sana, mambo yafuatayo ndio vyanzo vikuu vya tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume:-
• Upigaji punyeto wa muda mrefu.
• Msongo wa mawazo.
• Ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu (pressure).
• Kupooza kwa mwili.
• Kuugua ugonjwa wa ngiri.
• Kuugua chango la kiume.
• Ulevi uliokithiri.
• Kuwa na wasiwasi wa kumudu kutekeleza tendo la ndoa.
• Woga wa kufanya tendo la ndoa.
• Uzoefu wa kukatisha tamaa wa siku za nyuma.
• Ulaji mbovu wa vyakula haswa vyenye mafuta mengi/kupita kiasi.
• Mazingira yasiyoridhisha wakati wa tendo la ndoa.
• matumizi ya madawa makali (hususani madawa ya kizungu) ya kuongeza nguvu za kiume, husababisha mishipa ya uume kulegea Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
• Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone.
• Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini.

Kutokuwa na nguvu za kiume huleta madhara na athari nyingi sana kwa muhusika. Baadhi ya athari hizo ni pamoja na:-
• Kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi.
• Kuvunjika kwa ndoa.
• Kujiua: Baadhi ya wanaume hufikia uamuzi wa kujiua baada ya tatizo kuwa kubwa na kutumia dawa za aina mbalimbali bila mafanikio.


• Upungufu wa nguvu za kiume huongeza chachu ya maambukizi ya V.V.U kwa wanandoa: Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linapokuwa sugu, hupelekea rafiki wa kike/ mke wa mwanaume anaye sumbuliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, kutoka nje ya ndoa kwa ajili ya kutimiziwa haja zake za kimwili, mwisho wa siku mwanamke huyo huweza kumletea magonjwa mume wake mwenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume pindi wanapokutana kimwili katika hali hiyo hiyo ya kutoridhishana.


• Ulevi kupita kiasi; Wakati mwingine wanaume wanao sumbuliwa na tatizo hili, huamua kuwa walevi kupita kiasi ili angalau kupunguza mawazo. 


Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi sio lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. 


Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster".CHANZO:http://darasanileo.blogspot.com/
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: