MAADUI ZAKO NAMNA WANAVYOWEZA KUKUVUSHA KATIKA HATARI KWA NJIA YA CHUKI YA KUKUMALIZA
Siku moja punda wa mkulima mmojaalidondoka ndani ya kisima. Punda huyo alilia kwa sauti ya uchungu kwa masaa kadhaa huku
mkulima akitafuta namna ya kufanya, Mwisho akaamua, kwanza punda huyo alikuwa keshazeeka na kisima hicho kilitakiwa kifukiwe ; hivyo hakuona shida kumfukia punda huyo kisimani.
Aliamua kuwaalika majirani zake wote waende kumsaidia. Walichukua chepeo zao na kuanza kurusha udongo na takataka kwenye kisima hicho.
Mwanzo kabisa punda aligundua kinachoendelea na kulia kwa sauti kuu. Kutokana na mshangao wa kila mmoja wao, punda yule
alinyamaza kimya.
Jinsi walivyoendelea kutupa udongo baadaye, mkulima huyo aliangalia kisimani na kushangazwa na alicho kiona, kwa kila lundo la udongo lililogonga mgongoni mwa punda huyo, alikuwa akifanya kitu cha kushangaza.
Alikuwa akijitikisa na kujiinua kupanda juu.
Jinsi majirani wa mkulima huyo walivyoendelea kutupa udongo juu ya mgongo wa punda huyo, alichukua hatua kupanda juu.
Ghafla, kila mmoja alishangaa kuona punda amepanda juu ya kisima na kutoka nje.
Maana yangu ni hii;
Katika maisha, wako wengi watakao kuchukia na kukataa kukupa msaada unapohitaji.
Lakini kadiri wanavyo ongeza chuki kwako ndipo nawewe utajitahidi kupitia manyanyaso yao kujikwamua na mwisho kufika malengo yako.
Huenda wasingekuchukia usingeongeza jitihada na kuhakikisha unafanikiwa. Kila changamoto inayotupata ni njia ya kusonga mbele.
Na ili tuweze kutoka katika matatizo yanayo tupata, hatuna budi kupitia changamoto mbalimbali. Usikate tamaa wala kuona kwamba Mungu amekuacha, hapana ; elewa kwamba baada ya changamoto na magumu, mafanikio yanakuja.
UJUMBE KUTOKA KWA Emmanuel Gyuzi
0 comments:
Post a Comment