MADIWANI WATAKA VYOMBO VYA DOLA KUMTUMBUA JIPU MKURUGENZI WA GAIRO MOROGORO.
Madiwani wa Halmashauri ya Gairo wameziomba mamlaka husika kumchukulia hatua Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Mbwana Maguto kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi hali iliyosababisha miradi yote inayotekelezwa katika halmashauri hiyo kuwa chini ya kiwango.
Hata hivyo, Maguto hakuwa tayari kuzungumza madai hayo kwa madai kuwa yote yameshazungumzwa kwenye kikao.
Wakizungumza katika baraza maalumu la madiwani mwishoni mwa wiki walisema halmashauri yao imepokea zaidi ya Sh1.5 bilioni kutoka serikalini kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, barabara na afya lakini miradi hiyo imeshindwa kuleta tija kwa wananchi kutokana na kutokamilika na mingine kukamilika kwa kiwango duni.
Akizungumza katika kikao hicho Diwani Kibedya,Mangapi Mdangu alisema kuwa mradi wa maji Kibedya ulianza mwaka 2014 na umegharimu Sh502 milioni fedha kutoka benki ya dunia lakini mradi huo uliozinduliwa na mwenge mwaka 2015 ulitoa maji siku tatu tu na baada ya hapo maji hayakutoka tena na walipofuatilia kwa mkurugenzi waliambiwa mashine ya kusukumia maji imekufa wasubiri fedha zipatikane itanunuliwa nyingine.
“Huu ni mradi wa mamilioni ya fedha lakini hauna tija yoyote kwa wananchi, kwanini halmashauri ishindwe kumchukulia hatua mkandarasi ambaye anakabidhi mradi ambao mashine yake ni dhaifu na imeshindwa kufanya kazi, mkurugenzi ameshindwa kutupa ufafanuzi," alisema Mdangu.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment