Mratibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (Moropc) Thadei Hafigwa wa kwanza kulia akiwa sambamba na wanafunzi wa kozi ya uandishi wa habari kutoka vyuo mbalimbali vya habari na mabango yenye ujumbe mahususi wakati wa maandamano ya kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yaliyoanzia Shan Sinema na kumalizikia ofisi za chama hicho mtaa wa Nunge Manispaa ya Morogoro jana Mei 3 mwaka 2016. PICHA/MTANDA BLOG
Mwenyekiti mstaafu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (Moropc) Aziz Msuya kushoto akiwa amebeba bango na mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari cha Greenbert Polytechnc College Morogoro likiwa na ujumbe mahususi wakati wa maandamano ya kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yaliyoanzia Shan Cinema na kumalizikia ofisi za chama hicho mtaa wa Nunge Manispaa ya Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG
Askari wa kikosi cha usalama barabara akiongoza maandamano hayo.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari cha Morogoro (MSJ) wakiwa na bango lenye ujumbe wa kilele cha maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani wakati wa maandamano hayo.PICHA/MTANDA BLOG
Hawa ni sehemu ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari cha St Joseph College Morogoro
Sehemu ya waandishi wakongwe wakiwa kwenye maandamano hayo.
Mratibu wa chama cha waandishi wa habari Morogoro Thadei Hafigwa akizungumza jambo kwa wanafunzi wa kozi ya uandishi wa habari kutoka vyuo mbalimbali makao makuu ya chama hicho mtaa wa Nunge. PICHA/MTANDA BLOG
Mmoja wa waandishi wa kituo cha redio cha Redio Ukweli FM akiwa na bango baada ya kumalizika kwa maandamano hayo.PICHA/MTANDA BLOG
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (Moropc) Nickson Mkilanya (katikati) akizungumza jambo makao makuu ya chama hicho baada ya kumalizika kwa maandamano, kushoto ni Mkuu wa chuo cha waandishi wa habari Morogoro (MSJ) Nongwe S. Nongwe na kulia ni Katibu msaidizi wa chama hicho, Jimmy Mengele.PICHA/MTANDA BLOG
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment