BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIJIJI VYA WILAYA YA KILOSA VYANYEMELEWA NA JANGA LA NJAA MOROGORO.


 

Na Lilian Lucas, Morogoro 
Vijiji viwili vya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro huenda vikakumbwa na njaa baada ya mashamba yao kudaiwa kugawiwa kwa wageni.

Vijiji hivyo ni vya Mvua na Gongwe vilivyoko katika Kata na mashamba hayo ya mpunga ambayo yako katika mradi wa skimu ya umwagiliajia, yanafikia ekari 1,320.

Taarifa za uvamizi huo zimeshatolewa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, John Henjewele, alipofanya mkutano wa hadhara na wanavijiji hao.

Wamemwambia mkuu huyo wa wilaya kuwa mradi ulianzishwa kwa masharti ya kutumiwa na wakazi wanaozunguka eneo hilo, kinyume na hali ilivyo sasa.

Wanavijiji hao wameulaumu uongozi wa umoja wa wakulima wa umwagiliaji (Uwaumvu) ulioamua kuamua kuyagawa mashamba hayo bila kuwapa taarifa.

Kutokana na tuhuma hizo, Henjewele ameamua kuuvunja uongozi wa umoja huo na ameagiza kuanzia sasa mradi huo usimamiwe na wataalamu wa kilimo wa wilaya na kijiji, wakiongozwa na ofisa ardhi wa wilaya hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: