WALIMU WAKIONA CHA MTEMA KUNI BAADA YA KUTEMBEZEWA KICHAPO NA KUKUNG'UTWA NA WAFUGAJI BAADA YA KUWAZUIA WASICHUNGIE MIFUGO YAO ENEO LA SHULE
Picha ya maktaba mwalimu akifundisha wanafunzi darasani
Bariadi. Walimu watano wamepigwa na kung’olewa mazao yao mashambani na wanakijiji kwa madai ya kuwazuia kuchungia mifugo katika maeneo ya shule.
Katibu wa Chama cha Walimu nchini (CWT) wilayani hapa, Baraka Owawa amewaambia waandishi wa habari baada ya kutokea tukio la kati shule za msingi Giriku, Nkindwabiye, Sapiwi na Nyamikoma.
Owawa amewataja walimu waliopigwa na wananchi kwa madai ya kuzuia mifungo kufanya malisho katika maeneo ya shule kuwa ni Masumbuko Jackson, George Mwakanusya, Joseph Marco, Zacharia Jeremiah na Hipolitus Domisian ambao walilazimika kukimbia vituo vyao vya kazi.
Amesema licha ya kupigwa, walimu hao wamepewa vitisho na wanakijiji wanaojiita wazawa kuwa wanaweza kusingiziwa kuwabaka wanafunzi au kutembea na wake za watu ili kuhalalishiwa tuhuma za kuwapiga.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment