BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI (GESTI) NA HOTELI KUSITISHA KUTOA HUDUMA KISA MLOLONGO WA KODI IRINGA.

Iringa. Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Nyumba za Kulala Wageni na Hoteli mkoani Iringa (Iloha) Adam Lameck amesema wafanyabiashara wa huduma hizo wamekataa kulipa tena ushuru wa hoteli hadi watakapoonana na uongozi wa mkoa.

Akizungumza leo katika mkutano wao alisema watalazimika kusitisha utoaji huduma kutokana na mlolongo wa kodi.

“Endapo hatutasikilizwa, tunafunga biashara zetu mpaka hapo tutakapopata muafaka,” alisema.

Mmiliki wa Nyumba ya Wageni, Zakaria Mdeka alisema tangu mwaka 2008 kodi hiyo ilifutwa lakini wao waliendelea kulipa kwa asilimia 10 bila kuzingatia mmiliki anaingiza shilingi ngapi.

Wafanyabiashara hao wamedai wamekuwa wakitozwa mlolongo mkubwa wa kodi zaidi ya 23 ambazo zote zinatakiwa kulipwa bila kuzingatia mmiliki anapata faida kiasi gani.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: