Picha ya maktaba askari wakiwa katika majukumu yao.
JESHI la Polisi katika mkoa wa Dodoma limeanza kuweka mikakati kabambe ya usalama kwa askari zaidi ya 200 kufanya doria mchana kwa kutumia magari 27 ili kujiweka sawa katika kukabiliana na vurugu zozote zitazoweza kutokea mkoani humo.
Kwenye mitaa ya Dodoma, jana asubuhi askari zaidi ya 200 wakiongozwan na Kamanda wa Polisi mkoani huo, Lazaro Mambosasa walifanya doria na mazoezi kwa vitendo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lazaro Mambosasa alieleza kuwa hali hiyo ni kazi ya kuuweka sawa mkoa wa Dodoma kutokana na tetesi za uwepo wa watu kufanya vurugu siku za usoni.
Mambosasa alieleza kuwa doria kama hizo huwa zinafanyika usiku, lakini kwa sasa jeshi hilo limeamua kufanya mchana na walikuwa wanajaribisha kama vyombo vya vipo vizuri na kuwa hilo ni zoezi la kawaida.’
"Hatukuwa na doria ya kutembea kwa miguu tuliamua kutumia pikipiki na sehemu ya magari yetu kuuweka mji katika hali ya usalama,” alisema.
Kamanda huyo alieleza kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuendelea kufanya wakazi wa Dodoma kuendelea kuwa na hali ya usalama ambapo mkoani huo ndio makazi makuu ya Serikali na Chama kinachotawala dola.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment