Baadhi ya vijana wa mtaa wa Magereza Veta kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro wakisomba mabomba yaliyotolewa na mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood 80 yenye thamani ya sh7 milioni kwa ajili ya kuvuta maji eneo hilo linalokabiliwa na changaoto ya upungufu wa majisafi na salama
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood akizungumza na wananchi wa mtaa wa Magereza Veta kata ya Kihonda baada ya kukabidhiwa mabomba 80 yenye thamani ya sh7 milioni ili yatumike kuvuta maji kutokana ambapo kata hiyo hupata mgao wa maji mara moja ndani ya sikutano. Wachuuzi wa matunda katika Manispaa ya Morogoro wakiwa wamebeba mabeseni yenye mapapai wakipita eneo la Masika wakati wakisaka wateja wa kuwauzia matundani hayo ambapo papai moja huuzwa kati ya Sh800 hadi Sh3,000 kulingana na ukubwa wake.Mabasi madogo yakiwa yameegesha eneo la Masika Manispaa ya Morogoro huku yakipakia abiria kinyume na ilani inayozuia eneo hilo likiwa ni kwa ajili ya kupakia na kushusha tu na sio kituo cha mabasi.PICHA/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment