WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA URENO WAKENUA MENO NA KOMBE LA MATAIFA YA ULAYA 2016.
Nahodha wa timuu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo akiwa amenyanyua kombe la ubingwa wa kombe la mataifa ya Ulaya 2016 baada ya kuifunga Ufaransa bao 1-0 katika fainali ya michuano hiyo katika muda wa nyongeza wakati wakirejea katika ardhi ya Ureno leo asubuhi.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ureno wakiwa katika picha ya pamoja na kombe la Euro 2016 kabla ya kurudi nyumbani leo.
Cristiano Ronaldo akiwa katika pozi na kombe la michuano ya Euro 2016.t
Ronaldo akiwa amenyanyua kombe la ubingwa wa mataiafa ya Ulaya kwa mwaka 2016 wakati wakirejea nyumbani kutoka nchini ufaransa yalikofanyika mashindano hayo.
Ricardo Quaresma akiwa amebeba kombe hilo baada ya timu ya taifa kulitwaa kombe hilo katika michuano ya Europee nchini Ufaransa
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno, Fernando Santos (mwenye kombe) akiwa na kombe na nahodha wa timu hiyo, Christiano Ronaldo wakati wakirejea nyumbani kutoka Ufaransa katika michuano ya EURO 2016 kufuatia kuishinda timu ya taifa ya Ufaransa bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo katika dakika ya nyongeza jana usiku.
Basi lililowabeba wachezaji wa timu ya taifa ya Ureno likitoka uwanja wa ndege wakati wakitoka Ufaransa.
Mchezaji wa akiba, Eder aliyefunga bao pekee katika mchezo wa fainali kombe la EURO dhidi ya wenyeji Ufaransa kwa bao 1-0 akiwa amebeba kombe hilo, huku nahodha wa timu hiyo Ronaldo na Luis Nani wakifurahia jambo wakati wakiwasiri nyumbani Ureno leo asubuhi
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno, Fernando Santos (mwenye kombe) akiwa amenyanyua kombe mara baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ufaransa katika mchezo wa fainali wa kombe la EURO 2016 nchini Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment