WAUMINI WA KIKE WA DINI YA KIISLAMU WAONYWA NA MAVAZI
MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete akisalimiana na waumini baada ya swala ya Idd el Fitr, Julai 6 mwaka huu katika msikiti wa Al Farouq, Kinondoni, Dar es Salaam.
Waislamu wametolewa wito kuongeza subira na kuelewa kuwa kila penye uzito na wepesi hufuatia.
Wito huo ulikuwa moja ya ujumbe katika khutba ya Iddul fitr iliyotolewa kwenye viwanja vya Tangamano jijini Tanga kuadhimisha kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani 1437 hijriya sawa na mwaka 2016 julai 6.
Katika khutba hiyo iliyokuwa na nukta sita iliyotolewa na sheikh Salim Bafadhili,waislamu kwanza walitakiwa kumtukuza zaidi Mwenyezi Mungu kwa kuleta takbira na kuendeleza kila wema waliokuwa wakiutenda katika mwezi mzima wa Ramadhani.
Nukta ya sita iliwahusu zaidi wanawake ambao kwa mara nyengine sheikh Salim aliwahimiza kuongeza ibada ya utoaji sadaka na kujisitiri kwa kununua mavazi yanayokubaliana na imani yao.
Tofauti na khutba za iddi za miaka ya nyuma waumini kwenye viwanja hivyo wameonekana kujaa zaidi jambo linaloweza kuchangiwa na siku hiyo kuangukia siku moja kwa dunia nzima.
Jambo liliokuwa wazi ni kwamba waislamu walisubiri kusikia mwito wa masheikh wao kuhusiana na suala la usalama hasa baada ya minong’ono kuwa mingi mitaani juu ya watu kutekwa nyara baadhi wakipatikana wamekufa kwa majeraha ya risasi na wengine hadi sasa wakitafutwa na ndugu zao bila mafanikio.
Kuhusiana na nukta hiyo iliyokuwa ya tano,sheikh Salim aliwataka waislamu kuongeza subra na kuwacha kukurupuka na wajuwe kwamba kila penye shari na kheri hufuatia.
Alisema kuiwacha subra kutawapatia sababu zaidi wale wenye kuwatesa na ama kuuwa waislamu kwa njia ya kuwachinja au kuwapiga risasi kwenye mji huu na miji mengine nchini.
Akifafanua,sheikh Salim alisema yale yanayowakuta waislamu mara nyingi inachangiwa na yale yanayochumwa na mikono yao.
Akasema ni kweli wapo vijana wenye tabia za viashiria vya shari hata hivyo akasema jambo hilo halihalalishi kuuwawa kwa watu kwa namna hizi kwani vyombo vya sheria vipo.
Akimalizia nukta hiyo,sheikh Salim alitoa wito kwa masheikh wenzake wanaoongoza waislamu nchini kukutana pamoja ili waonane na vyombo vya usalama vya kitaifa ili wakaulizie wapi tunakoelekea na lini yatakwisha mambo hayo.
Kuhusiana na mwenendo huo wa mauwaji ya kimya kimya,sheikh Salim alionyesha hofu yake kwamba pindi yakiendelea yanaweza yakazalisha visasi kwani kila aliyepotelewa na ndugu yake ni rahisi kuchukua maamuzi hayo.Chanzo:http://islamictides.com
0 comments:
Post a Comment