Askofu wa jimbo kuu la Morogoro, Telesphory Mkude/PICHA NA MTANDA BLOG.
Juma Mtanda, Morogoro
Askofu wa jimbo kuu la Morogoro, Telesphory Mkude ameeleza kuwa kila awamu ya kuongoza nchi inaanza na mwazo wake na rais John Magufuli katika kipindi cha mwaka mmoja watanzania wameshuhudia taifa ikijipatia manufaa baada ya kufumuafumua misufumo ya vigogo kujipatia fedha za udanganyika kupitia watumishi hewa na wanafunzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ibada ya krismasi kanisa kuu la St Patrice mkoani hapa, Askofu Mkude alisema kuwa rais Magufuli ameonekana ni mtu jasiri baada ya kufumua mifumo mbalimbali ya vigogo kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu lakini na kujenga nidhamu kwa watumishi wa serikali yake.
Serikali ilikuwa na wanafanyakazi hewa, wanafunzi hewa lakini kwa upande wa malipo fedha hazikuwa hewa na mishahara imelipwa kwa baadhi ya vigogo wasiowaamini na kunufaika nayo kutokana na udanganyifu wao katika utumishi wa serikali.alisem Askofu Mkude.
Askofu Mkude alisema kuwa utendaji kazi unaofanywa na rais Magufuli na wasaizidi wake unapaswa kuungwa mkono hasa kwa juhudi za kuwatumbua vigogo waliokuwa wametengeneza mradi wa kujipatia fedha kupitia wafanyakazi hewa na kujinufaisha na kulitia hasara taifa.
“Rais Magufuli anapaswa kupongezwa kutokana na tathimini ya mwaka mmoja tangu aingie madaraka, nathani taifa limepata kitu cha kujivunia na unaweza kujiuliza kwanini tuwe na watu wengi wasiofanya kazi na wanalipwa mishahara lakini huwezi kumuuliza Mgufuli, kwa sababu ameikuta hali hiyo na haikuonekana kama hali hiyo ni ya mwaka mmoja na hakukuwa na mtu wa kuzuia juu ya watumishi hewa..?”alihoji Askofu Mkude.
Askofu Mkude alisema kuwa kuna baadhi ya vigogo wamefaidika na suala la wanafunzi hewa pamoja na wafanyakazi hewa kwa kujipatia fedha kutoka serikali lakini katika maandiko matakatifu yanaeleza kuwa asiyefanya kazi na asile hivyo udanganyifu huo umefanyika na unapaswa kuzuia kwa nguvu zote.
“Kuna wanafunzi hewa lakini fedha zilizotolewa hazikuwa fedha hewa huo ni udanganyifu na wengine wamefaidika kwa sababu sio haki yao kwani walikuwa wanafanya kama utaratibu wa kawaida kumbe sio hivyo wanapaswa kusahihishwa.”alisema Askofu Mkude.
Aliongeza kuwa sasa hivi baadhi ya wafanyakazi katika wilaya na mikoani kasi yao ya utendaji kazi imebadilika lakini inatokana na kila mtu kuchunga kazi yake asije kutumbuliwa na kuharibu kibarua, hiyo ndio nidhamu inayotakiwa kuwepo kwa watumishi wa mungu na serikali.
Askofu Mkunde alisema kuwa kitendo cha rais Magufuli kuzuia fedha kwa ajili ya sherehe za kitaifa na fedha hizo kubadilishwa matumizi ni jambo la kujivunia kutoka kwa kiongozi huyo kwani tumeshuhudia na kuona ujenzi wa barabara ya Mwenge jijini Dar es Salaam, vitanda vikinunuliwa na kupelekwa hospitali ya taifa ya Muhimbili na mambo nyingine mazuri yakifanyika na wananchi wajasikia fedha zimeingia katika mifuko ya rais.
Kama kuna mapungufu ambayo yameonekana kwa kiongozi huo yanapaswa kukosolewa kwa njia sahihi lakini pale alipofanya vizuri panafaa kupongezwa lakini bila shaka umma ulishangwa na kitendo cha mke wa rais kulazwa hospitali ya Muhimbili wakati anaumwa badala ya kupelekwa nje ya nchi kutibiwa.alisema Mkude.
0 comments:
Post a Comment