BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HIVI NDIVYO KRISMASI ILIVYOADHIMISHWA 2016 MOROGORO NA TASWIRA YAKE NDIO HII.


Askofu wa jimbo kuu kanisa katoliki Morogoro, Telesphory Mkude akitoa baraka kwa mmoja wa watoto waliohudhuria ibada ya sikukuu ya krismasi katika kanisa kuu la katoliki la St Patrice Morogoro.PICHA ZOTE NA MTANDA BLOG.
Askofu wa jimbo kuu la kanisa katoliki Morogoro, Telesphory Mkude akitoa sakalamenti wakati wa ibada ya sikukuu ya krismasi katika kanisa kuu la katoliki la St Patrice Morogoro.
Muunguzi wa zamu katika wodi ya wazazi ya hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro, Mariamu Mazengo akimkadhi mtoto Bi, Prisca Severine (23) baada ya kujifungua katika mkesha wa sikukuu ya krismasi kwenye hospitali hiyo ambapo jumla ya watoto 25 walizaliwa. Mkuu wa nidhamu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Morogoro, Muungano Nassoro akizungumza na abiria ndani ya moja ya basi juu ya umuhimu wa kufunga mikanda ya usalama.

Afande huyo aliwataka abiria hao kutoa taarifa endapo dereva wa basi anakeuka sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali walipokuwa wanapoita stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ya Msamvu Morogoro.Afande Muungano Nassoro akiendelea kutoa elimu kwa abiria kabla ya kuwageukia makonda madereva kuendesha gari kwa kuzingatia sheria za usalama barabara ili kuepusha ajali.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa kando ya barabara ya Makongoro Manispaa ya Morogoro huku wakiwa wamepanga mapambo ya aina mbalimbali wakati wakisubiri wateja wao kununua kwa ajili ya kupamba katika nyumba zao ili kusherehekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya 2017.

Juma Mtanda, Morogoro.
Jumla ya watoto 29 wamezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya krismasi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na kituo cha afya Mafiga mkoani hapa.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Muuguzi wa zamu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Rebecca Lembile alisema kuwa katika mkesha huo jumla ya watoto 25 wamezaliwa huku watoto watatu wakizaliwa kwa wazazi wa kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Rebecca alisema kuwa katika idadi hiyo ya watoto 25, watoto wa kiume ni 14 na kike 11 huku wazazi watatu wakishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kulazimika kufanyiwa upasuaji.

“Mkesha wa krismasi kuna jumla ya watoto 25 waliozaliwa katika hospitali yetu na kati ya hao watoto wa kiume wapo 14 na kike 11 lakini ni wazazi 22 ndio waliojifungua kwa njia ya kawaida na wazazi watatu walishindwa kujifungua njia ya kawaida na kufanyiwa upasuaji, watoto na wazazi wao wanaendelea vizuri tunashukuru mungu.”alisema Rebecca.

Kwa upande wa kituo cha afya Mafiga jumla ya watoto wanne wamezaliwa kwenye mkesha huo huku watoto wa kiume wakiwa wawili na kike wawili na hali za wazazi na watoto wao zikiendelea vizuri.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: