RAIS John Magufuli amewateua wakuu wa wilaya wawili na wakurugenzi 3 wa mamlaka za Serikali za Mitaa. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Kisare Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Humphrey Polepole ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi.
Mwanasheria maarufu Evod Mmanda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara iliyopo katika Mkoa wa Mtwara. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Khatib Kazungu ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Katika uteuzi huo, Rais Magufuli alimteua Ramadhan Mwangulumbi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga iliyopo mkoani Shinyanga.
Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Lewis Kalinjuna ambaye anastaafu kwa mujibu wa Sheria. Rojas Romuli ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iliyopo katika Mkoa wa Katavi. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ngalinda Ahmada aliyefariki dunia hivi karibuni.
Mwingine aliyeteuliwa ni Rashid Gembe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga iliyopo katika Mkoa wa Tanga, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mkumbo Barnabas ambaye uteuzi wake ulitenguliwa hivi karibuni.
"Uteuzi wa huu unaanza mara moja na wateule wote wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mara wapatapo taarifa hii," ilisema taarifa ya Ikulu.
Kairuki atangaza 27 kuwa ma DAS Wakati huo huu, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angella Kairuki jana alitangaza uteuzi wa makatibu tawala 27 ambao wameteuliwa kujaza nafasi mbalimbali zilizokuwa wazi.
Walioteuliwa kushika wadhifa wa katibu tawala ni Timotheo Mzava (Arumeru), Fabian Sospeter (Nyang'wale), Innocent Nsena (Karagwe), Abdallah Mayomba (Misenyi), Greyson Mwengu (Kyerwa), Agnes Alex (Biharamulo), Mbwana Kambangwa (Liwale), Agenelius Mwakitalu (Kilwa), Sarah Sanga (Hanang), Paul Bura (Mbulu), Yohana Kasitila (Kilosa) na Robert Selasela (Kilombero).
Wengine ni Lameck Lusesa (Malinyi), Palangyo Abdul (Nyanyumbu), Bosco Bugali (Misungwi), Menruf Nyoni (Magu), Said Kitinga (Ilemela), Grace Mgeni (Makete), Zaina Mlawa (Ludewa), Milongo Sanga(Kibiti), Frank Sichalwe (Kalambo), Nicodemus Mwikozi (Meatu), Filbert Kanyilizu (Itilima), Godwin Chacha (Busega), Winfrida Funto (Ikungi), Elizabeth Rwegasira (Mkalama) na Michael Nyahenga (Kaliua).HABARILEO
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ RAIS MAGUFULI AENDELEA KUIMARISHA SERIKALI YAKE KWA KUTEUA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment