BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WEZI WAVUNJA OFISI YA KATIBU TAWALA WILAYA NA KUIBA KOMPYUTA MBILI USIKU LINDI

WATU wanaosadikiwa kuwa wezi, wamevunja ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi na kuiba kompyuta mbili zenye thamani ya Sh. milioni mbili.

Habari zilizopatikana jana kutoka vyanzo mbalimbali na kuthibitishwa na uongozi wa wilaya hiyo na Jeshi la Polisi, zilisema wizi huo ulitokea katikati ya wiki hii.

Baadhi ya watoa habari (majina yao yanahifadhiwa) walisema jana mjini hapa kuwa kutokana na wizi huo, watumishi wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea, Stephen Mbije, alipoulizwa juu ya tukio hilo, alikiri kutokea kwa wizi huo na kueleza kuwa taarifa zake zimefikishwa polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

“Hizo taarifa za wizi wa vifaa ni kweli na tayari zimefikishwa polisi katika kituo kikuu cha polisi wilaya na wanaendelea kuzifanyia kazi,” alisema Mbije.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mohamed Likwati, alithibitisha kutokea kwa wizi huo aliosema ulifanywa na watu wasiofahamika. Alisema kutokana na tukio hilo, watumishi wawili wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na upotevu huo.

Amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Ally Mohamed (57), mhudumu wa ofisi na Magreth Philipo (46) mtunza kumbukumbu, wote wakiwa wafanyakazi wa ofisi hiyo ya wilaya. “Hizo taarifa ni za kweli, hivyo hadi tunazungumza na wewe hii leo (jana) hawa watumishi tunaendelea kuwashikilia kwa mahojiano zaidi,” alisema.


Likwati na kuongeza kuwa watumishi hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kukamilika upelelezi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: