BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMPUNI YA SIMU YA TTCL YAIPIGIA MAGOTI KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MOROGORO

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt Steven Kebwe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma ya teknolojia ya kisasa ya internet ya 4G-LTE kwa mkoa huo iliyozindua katika ofisi za kamouni ya simu Tanzania eneo la Posta, kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba.

Juma Mtanda, Morogoro.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro imeombwa kusaidia kudhibiti vitendo vya hujuma vinavyofanywa na baadhi ya watu dhidi ya miundombinu ya kampuni ya simu Tanzania (TTCL) huku hujuma hizo zikitajwa kuathiri na kurudisha nyuma kwa kiasi kubwa kukua kwa uchumi wa nchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya teknolojia ya kisasa ya internet ya 4G-LTE kwa mkoa wa Morogoro, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema kuwa hujuma zinazofanywa na baadhi ya watu zimekuwa zikirudisha nyuma juhudi na kasi za kutoa huduma kwa jamii.

Kindamba alisema kuwa kampuni hiyo ipo katika utekelezaji mkakati wa biashara ya miaka mitatu iliyoanza mwaka 2016-2018 kwa lengo la kuboresha na kuleta huduma mpya katika soko la teknolojia hapa nchini.

“Kwa sasa TTCL imekuja na kasi mpya kupitia teknolojia ya kisasa ya internet ya 4G-LTE na leo (jana) tumezindua katika mkoa wa Morogoro lakini ombi letu ni kuiomba kamati ya ulinzi na usalama na vyombo vingine vya dola itusaidie kuwashughulikia kikamilifu baadhi ya watu wanaohujumu mbiundombinu ya mawasiliano yetu.”alisema Kindamba.

Kindamba alisema kuwa TTCL ipo katika mpango endelevu wa kuwezesha kufanya mabadiliko ya msingi na kurejesha huduma za mawasiliano katika nyanja zote kwa kishindo kikubwa katika soko la mawasiliano na kuleta huduma bora Tanzania.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt Steven Kebwe na Kaimu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba wakinyanyua mabango yenye ujumbe Fii" Morogoro Mlamkaa! Tumefanikiwa wakati wa uzinduzi wa huduma ya teknolojia ya kisasa ya internet ya 4G-LTE 

Naye Meneja Mawasiliano wa TTCL makao makuu, Nicodemus Mushi alisema kuwa kwa sasa kampuni hiyo ipo katika maboresho makubwa ili iweze kutoa huduma bora zaidi hapa nchini ambapo awamu ya kwanza itahusisha katika miji mikuu na maeneo muhimu.

Mushi alisema kuwa katika awamu ya kwanza, kampuni ya simu Tanzania itatoa huduma ya teknolojia ya kisasa ya internet ya 4G-LTE katika miji mikuu na baadaye huduma hiyo itafika katika katika miji ya wilaya na vijijini ifikapo Desemba mwaka huu.

“Huduma hii ya teknolojia ya internet ya 4G-LTE itawafikia watanzania wote ifikapo Desemba 2017 katika miji mbalimbali za Tanzania lakini kwa sasa tupo katika awamu ya kwanza ambapo awamu hii itafikia wale wa miji mikuu, taasisi za elimu ya juu na vituo vya utafiti.”alisema Mushi.

Mushi alisema kuwa TTCL ili kuboresha zaidi mawasiliano ya huduma ya mawasiliano tayari TCRA imetoa kibali cha kuzima masafa ya CDMA ifikapo Februari 30 mwaka huu na kupatiwa huduma ya kisasa zaidi ya masafa ya 800Mzh itayosaidia kusambaza huduma hiyo kwa haraka zaidi.

Baada ya kuzindua huduma hiyo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt Steven Kebwe alisema kuwa TTCL kwa sasa ina jukumu kubwa la kuhakikisha inarejesha wateja waliokuwa wamehama kufuatia huduma za kampuni hiyo kudorora.

“Kuzinduliwa kwa teknolojia hii ya kisasa ya internet ya 4G-LTE sasa iwe chachu ya kuwarejesha wateja wote waliokuwa wamekimbia na kukimbilia mitandao mingine.”alisema Dkt Kibwe.

Gharama zenu ni ndogo lakini hofu yangu kuwa je endapo wananchi watagundua unafuu huo na kujiunga na huduma zenu mmejipanga vipi hapo ?.Aliongeza.

Dkt Kebwe alisema kuwa kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro ipo tayari kuhakikisha inawasaka watu wote wanaojihusisha kuhujumu miundombinu ya kampuni ya mawasiliano ya simu ya TTCL na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.

Kama utakamatwa na kukutwa na makosa ya kuhujumu miundombinu ya mawasiliano Tanzania utafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na kifungo chake ni maisha hivyo natoa raia kujiepusha na vitendo vya uhujumu.aliongeza.Dkt Kebwe.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: