BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

FRANCIS CHEKA KUKATA NGEBE ZA SAIDI MBELWA KATIKA MASUMBWI UWANJA WA JAMHURI MORO

Francis Cheka (SMG) kulia na Said Mbelwa (Moto wa Gesi) baada ya kupima uzito Coco Beach mtaa wa Makongoro Morogoro/MTANDA BLOG

Juma Mtanda, Morogoro.

Mabondia Francis Cheka (SMG) na mpinzani wake, Said Mbelwa (Moto wa Gesi) wamepima uzito huku kila mmoja akitamba kumdondosha chini mpinzania wake katika pambano kali la masumbwi la uzito wa kg 75 kwa kg76 la raundi 10 lisilo la ubingwa litakalofanyika kesho (leo Mei 6) katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

wakizungumza na gazeti hili mjini hapa mara baada ya kupima uzito kwa upande wa Cheka (kg 75) alisema kuwa atanachoka kwa sasa ni heshima na atautumia mchezo huo kurejesha makali yake mbele ya Mbelwa na kuwapa burudani ya kutosha mashabiki wake.

Cheka alisema kuwa anamfahamu vizuri mpinzani wake udhaaifu wake na kuwaondoa hofu mashabiki wajiandae kupokea ushindi.

“Mbelwa ni bondia nzuri hapa Tanzania lakini uzuri wake sio ni kwa manondia wengine lakini sio kwangu nitamtwanga ili awe na chakusimulia katika uzee wake.”alisema Cheka.

Kwa upande wa bondia, Saidi Mbelwa (76) alisema kuwa amekubali kucheza na Cheka kwa lengo moja tu la kuwadhihilishia mashabiki wa ngumi kuwa yeye ni bondia mkali hivi sasa Tanzania.

“Cheka amekuwa akinikimbia kwa muda mrefu kucheza na mimi lakini safari hii amekubali na sitaweza kufanya makosa zaidi ya kuwadhibitishia mashabiki kuwa nini ni zaidi ya mabondia hapa Tanzania baada ya kumtwanga.”alisema Mbelwa.

Naibu Katibu mkuu wa chama cha ngumi cha TPBO, Sais Chaku alisema kuwa katika pambano hilo litajumuisha mapambano ya utanguzi sana katika uzito tofauti.

Chaku alitaja pambano ya utangulizi na uzito wake katika mabano kuwa ni pamoja na Twaha Kassim (64) dhidi ya Shabaan Lambo (62.8), Ajibu Salum (60.5) mbele ya Kassim Said (62.5) na Epson John (61) dhidi ya Charles Chilala (59.8).

Wengine Maxmilian Maxmilian (67.5) atayecheza na Moris Mapunda (69), Joseph Malichou (73) na Gift Ngulumbi (75.7), Ally Hamis (56.5) dhidi ya Kudura Tamimu (57) huku Mwinyi Omary (53) na Hamza Mchanjo (51) wakati Nassib Msafiri (71) na Fred Justin (42) wakikosa wacheza wenye uzito sawa.alisema Chaku.

Mdhamini wa pambano hilo, Ibrahim Nyange alisema kuwa michezo ya utangulizi itaanza kuchezwa majira ya saa 12 jioni huku viingilio vikiwa sh10,000 kwa VIP na sh5,000.

"Kesho (Leo) tunataka kuona pambano kali la usiku wa mabingwa Tanzania kati ya Cheka na Mbelwa lakini mabondia chipukizi watapata fursa ya kujifunza kwa vitendo kutoka kwa nguli hawa wa masumbi kwa sasa hapa Tanzania".alisem Nyange.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro, Urlich Matei aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa jeshi hilo limejipanga kuhakikisha linaimarisha ulinzi na usalama kwa mashabiki wataodhuria pambano hilo.

Kamanda Matei alisema kuwa kutakuwa na askari wa kutosha na askari wa polisi jamii watakuwepo ili kuhakikisha mchezo huo unamalizika salama.

“Tunaimarisha ulinzi wa kutosha katika pambano hilo lakini kwa kikundi cha watu ama mtu mmoja mmoja wataodhubutu kuvunja amani kwa namna yoyote ile atachukuliwa hatua kali za kisheria.”alisema Kamanda Matei.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: