Ajali mbaya ya gari imetokea kaskazini mwa Tanzania ambapo basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia Karatu na kuua watu 32 mkoani Arusha.
Mkasa huo umetokea takribani kilomita 25 kutoka katika geti la hifadhi ya taifa ya Ngorongoro na zaidi ya kilomita 150 kutoka mji wa Arusha.
Wanafunzi hao walikuwa wamesalia na kilomita 5 ili kufika sehemu waliokuwa wakielekea.
Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mwalimu ilisema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi na walimu wanaosadikiwa kuwa thelathini na tano.
Mwandishi wa BBC mjini Arusha, Ally Shemdoe, aliyeko mkoani humo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mvua kali inayoendelea kunyesha katika eneo hilo.
Anasema kwamba dereva alidaiwa kutoijua barabara hiyo hivyobasi alikosa mweleko na kuteleza kando ya barabara kabla ya kutumbukia korongoni katika mto Malera. Raia wakiwa wamekusanyika katika shuleni hapo
Wanafunzi na waalimu hao walikuwa safarini kuelekea Karatu kwenye shule ya Tumaini English Medium Junior Schools kufanya mtihani wa kanda wa majaribio ya kujipima uwezo kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba wa Kanda.
Shule hizo mbili zimekuwa zikifanya utaratibu wao wa kawaida,
Taarifa kutoka katika hospitali ya Lutheran Karatu, kwa muujibu wa Mbunge Ester Mahawe aliyeko hospitalini hapo , ni kuwa maiti zilizopokelewa katika hospitali hiyo ni 32 hii ikiwa na maana , miongoni mwao waalimu wawili, dereva mmoja , na wanafunzi ishirini na tisa.
Kati ya wanafunzi waliopoteza maisha yao 10 ni wa kiume huku 18 wakiwa wasichana.
Aidha maiti zitahifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru.
Mkuu wa wilaya ya Arusha , Fabian Dagalo amewataka wananchi kuwa watulivu kutokana na tukio hilo baya, na kwamba serikali itatoa taarifa baadaye kuhusiana na msiba huo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ IDADI YA VIFOYA WANAFUNZI SHULE YA LACK VICENT WALIOTUMBUKIA KATIKA KORONGO MTO MARERA NA COASTAL WAFIKIA 32 ARUSHA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment