MMILIKI WA SHULE YA LUCKY VINCENT AKAMATWA KWA GARI LAKE KUHUSIKA KATIKA AJALI ILIYOUA WANAFUNZI 32 ARUSHA
MMILIKI wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha, Innocent Moshi anashikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo aliliambia MTANZANIA jana kwamba mmiliki huyo amekamatwa kutokana na gari lake kuhusika kwenye ajali iliyouwa wanafunzi 33, walimu wawali na dereva.
“Ni kweli tumemkamata, tunaendelea na upelelezi hayo mambo mengine ni taarifa zetu za upelelezi. Tukikamilisha na kumkuta ana hatia dhidi ya kilichotokea tutamfikisha mahakamani,” alisema Kamanda Mkumbo.
Taarifa za awali zinaeleza kwamba gari ya Mitsubishi Rossa T. 871 BYS mali ya shule hiyo ilihusika kwenye ajali hiyo ilikiwa inakwenda wilayani Karau huku ikiwa imebeba watu 39 badala ya 30.
Abiria waliokuwa kwenye gari hilo abao ni wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent walifariki dunia baada ya gari kuacha njia likiwa katika eneo la Mrera Rhotia wilayani Karatu kisha kupinduka na kuua wanafunzi 33, walimu wawili na dereva wa basi.
Ajali hiyo iliwaacha wanafunzi watatu waliokuwa ndani ya basi hilo, Godfrey Tarimo, Doreen Mshana na Sadia Awadhi wakiwa majeruhi ambao kwa sasa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha huku afya zao zikitajwa kuendelea kuimarika.
0 comments:
Post a Comment