BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WABUNGE CHADEMA FREEMAN MBOWE, HALIMA MDEE NA ESTER BULAYA NUSURA WASWEKWE SELO MJINI DODOMA

MJADALA mkali umeibuka bungeni leo mjini Dodoma baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kuwasilisha ripoti yake ya uchunguzi dhidi ya wabunge watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao wanadaiwa kudharau mamlaka ya spika kinyume cha kanuni za Bunge.

Wabunge waliochunguzwa na kamati hiyo walikuwa ni Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda) na mbunge wa Hai, Freeman Mbowe aliyesamehewa ambao wote wanadaiwa kufanya kosa hilo Aprili 4 mwaka huu wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Adhabu iliyopendekezwa na kamati hiyo dhidi ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ya kutakiwa afungiwe vikao vyote vya Bunge la bajeti ndiyo iliyozua mjadala bungeni na kulazimu wabunge wa Chadema na CCM kuungana pamoja kumtetea Mdee na Bulaya ambaye alipendekezwa apewe onyo kali.

Wabunge wa CCM waliomtetea Mdee asipewe adhabu hiyo ni Kangi Lugola, Peter Serukamba, Abdallah Bulembo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati kutoka Chadema ni Joseph Selasini (Rombo) na Riziki Shahari Mngwali kutoka CUF.

Waziri Mhagama ndiye aliyehitimisha mjadala huo kwa kutoa hoja ya kutengua dhabu zilziotolewa ili watuhumiwa wote wasamehewe akitumia kanuni ya 57 ya Bunge. 


Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika, alikubali ombi lililowasilishwa Mhagama na hivyo kutangaza kuwasamehe Mdee na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: