BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

17 WAKAMATWA NA POLISI WAKIPINGA MATOKEO JIMBO LA MVOMERO.


WATU 17 wakiwemo Diwani mteule wa kata ya Mtibwa kupitia chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Tusekile Mwakyoma na Mwenyekiti wa Wilaya chama hicho,Charles Mbaga wanashikiliwa na polisi katika kituo kidogo cha Turiani, wilayani hapa kwa madai ya kutaka kuandaa maandamano ya kupinga matokea ya uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 31.

Viongozi hao pamoja na wafuasi wengine wa chama hicho walipinga mgombea wa ubunge wa CCM Amos Makala kutangazwa mshindi wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro.
Walidai kuwa ushindi wa Makala hakuwa halali kutokana na kusisitiza kuwa kumekuwepo na wizi wa kura wakati wa zoezi zima la uchaguzi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Rehema Oden (67) ambaye ni mama mzazi wa Diwani mteule huyo alisema polisi walifika nyumbani kwake majira ya saa tisa alasili ya Novemba 3 na kuanza kuwapiga na kuwakamata watu hao.
Alisema katika kamata kamata hiyo ilimhusisha pia mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Mvomero, Charles Mbaga, mtoto wa diwani huyo na mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya Nasoro Seif , Evarenci Julius (16) ambaye hata hivyo aliachiwa baadaye.

Baada ya kukamatwa kwa viongozi hao sakata hilo liliendelea kwa jeshi la polisi kukamata watu wengine sehemu mbalimbali ambao wanadaiwa kuwa ni wananchama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambao walihusishwa na tuhuma za kutaka kufanya vurugu ikiwemo kufanya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Naye mmoja wa wanachama wa chama chicho, White Awadhi mkazi wa kijiji cha Kidundwe ambaye anadai kusakwa polisi alisema kuwa yeye tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu alikuwa muhamasishaji hali iliyosababisha wanachama wengi wa CCM kuhama na kuanza kukiunga mkono chama cha CHADEMA.

Alidai kuwa kitendo hicho huenda ndicho kilicho sababisha polisi kumsaka sambamba na kuandaa mipango ya kufanya maandamano ya amani kupinga kutangazwa kwa Makala kuwa ndiye mbunge mteule wa jimbo hilo.

“Mgombea ubunge wa Chadema alipata taarifa za kuwa wananchama na wananchi wanataka kuandamana lakini akiwa jijini Dar es Salaam alipiga simu ya kuzuia tusiandamane na sisi tulifuata maelekezo yake lakini cha kushangaza majira ya saa tisa alasiri mji wa Mtibwa tulivamiwa na askari wa kutuliza ghasia na kuwakamata Diwani na Mwenyekiti wa chama chetu”. Alisema Awadhi.

Alisema sababu za kutaka kuandamana kwa wananchama hao pamoja na wapenzi ni kunatokana na mgombe ubunge jimbo hilo kupitia Chadema, Matokeo Manyata kugundua kasoro nyingi zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura ikiwemo karatasi bandia.
“Mgombea wetu wa Chadema Matokeo Manyata kwanza amekamata karatasi bandia za kupigia kura na kasoro nyingine iliyojitokeza katika karatasi zile ni kuwepo kwa wino sehemu ambayo mgombea wetu aliwekewa alama ya ndiyo na kuweka wino kwa lengo la kuvuta,” Awadhi alisema.

Naye Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro, Ahmed Msangi akidhibitisha kukamatwa kwa watu hao alisema polisi haikumata wanachama wa Chadema isipokuwa wamekata wahuni.

“Kama unasema tumekamata wanachama wa Chadema lete majina yao na namba za kadi zao sikiliza polisi wamekamata wahuni na si wananchama wa Chadema kwani wananchama wa Chadema wapo makini” alisema Msangi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: