BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HALMASHAUR​I YA MANISPAA YA MORO YAKABILIWA NA CHANGOMOTO IKIWEMO UCHAFU KURUNDIKAN​A SEHEMU ZA KUHIFADHIA TAKANGUMU


Uchafu ukiwa umerundikana katika daraja lililopo eneo la Garilai kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro na kusababisha maji kushindwa kupitia kwenye mrefeji unaotoka mjini kwenda katika kumwaga maji mto Morogoro na kusababisha wakazi wa mtaa huo kuingiliwa na maji katika makazi yao yanayoshindwa kupita kiurahisi kwenye mfereji huo mkoani hapa.


HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro inakabiliwa na changamoto mbalimbaliikiwemo ya kurundikana kwa uchafu sehemu za kuhifadhia taka hali inayosababishakuwa kero kwa wakazi wa maeneo hayo hali inayosababishwa na ubovu wa magari yakuzolea takangumu.

Ubovu wa magari hayo yakubebea taka umesababisha kuwepo kwa uchafu mwingimaeneo mbalimbali ya kuhifadhia uchafu ikiwemo kata ya Kingo, soko kuu la mkoawa Morogoro na kata ya Mbuyuni.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa Mkurugenzi wa Halmashauri yaManispaa ya Morogoro, Javis Simbeyi alikiri kuwepo kwachangamoto hizo zikiwemo za kurundikana kwa uchafu katika maeneo ya kuhifadhi takahizo amabzo nyingi zimekuwa zikizalishwa kutokana na shughuli mbalimbali zakijamii amabpo zimekuwa zikikaa muda mrefu bila ya kuondolewa kupelekwa katikajalala kuu la taka.

Akifafanua juu ya changamoto hizoSimbeyi alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo tayari halmashauri yaketayari imeanza kufanya mikakati mbalimbali ya kulitatua tatizo hilo ikiwemo kukodimagari ya kwaajili ya kuziondoa taka hizo ambazo zimekuwa zikitoa harufu mbaya ya kuamsha manunguniko kwa jamii.

“ni kweli tumekuwa na changamoto mbalimbalindani ya halmashauri yetu lakini baadhi ya changamoto hizo tayari tumeanzakuzitatu hasa hii ya uchufu sehemu ya kuhifadhia uchafu tayari zoezi la kukodimagari kwa ajili ya kuziondoa taka hizo linafanyika hadi hapo magari yetuyatakapo tengemaa” alisema Sembeyi.

Aidha Sembeyi alisema kuwa kuhususuala la uwepo wa uchafu katika baadhi ya mifereji halmsahauri linalifanyiakazi hasa kwa sehemu za madaraja ambazo taka zimekuwa zikiziba na kusabaishakero kwa wakazi waliojirani na madaraja hayo kutokana na mitaro hiyo kushindwakupitisha maji kwa urahisi.

Aidha alisema kuwa halmashauriyake pia inafanya mikakati mbalimbali kwaajili ya kuwadhibiti machinga amabowameanza kufanya biashara katika maneneo mbalimbali kinyume cha sheria zahalmashauri amabo pia kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakisababisha uchafuzi wamazingira.

Sembeyi alisema halmashauriimekuwa na utaratibu wa kuwaondoa wafanyabiashara mara kwa mara katika maeneoyasiyoruhusiwa ila mwaka huu kumekuwa na changamoto nyingine hasa baada lasuala hilo kuingiliwa na siasa hivyo kushindwa kufanya kazi ya kuwaondoa nakudai suala hilo lipo kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kwa ajili ya utatuzi zaidi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: